MANCHESTER,
England
KLABU ya Manchester
United imetupilia mbali ofa ya Barcelona ya kiasi cha pauni milioni 45 ya kutaka kumnunua Paul Pogba pamoja na kuwatoa
Yerry Mina na Andre Gomes, kwa mujibu wa Sky nchini Italia. MANCHESTER,
England
KLABU ya Manchester
United imetupilia mbali ofa ya Barcelona ya kiasi cha pauni milioni 45 ya kutaka kumnunua Paul Pogba pamoja na kuwatoa
Yerry Mina na Andre Gomes, kwa mujibu wa Sky nchini Italia.
Taarifa hizo
zinafuatia ripoti ya awali kutoka kwa wakala wa Pogba, Mino Raiola, ambaye
alisafiri hadi mjini hapa katika jaribio la kutaka kumchukua mchezaji huyo wa
Man United ili kwenda kwa mabingwa hao wa Hispania kwa ajili kiungo huyo
Mfaransa.
Lakini United
kwa sasa haina mpango wa kuachana na Pogba, ambaye ndio kwanza amerejea katika
mazoezi baada na kushinda taji la Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 25, alisajiliwa na Man United mwaka 2016 – kwa ada
iliyokuwa rekodi ya dunia kwa wakati huo ya pauni milioni 93.25, na amebakisha
miaka mitatu katika mkataba wake wa sasa.
Hata kama
United itataka kumuuza mchezaji huyo, kesho Alhamisi ndio siku ya mwisho ya
dirisha la usajili la Ligi Kuu ya England, ambapo wana siku mbili tu kumpata
mchezaji atakayechukua nafasi yake.
Dirisha la
usajili halitafungwa Hispania hadi Agosti 31, hiyo ikiwa na maana kuwa Barcelona
wana nafasi hadi mwishoni mwa mwezi kujaribu kumsajili
Pogba (pichani) katika kipindi hiki cha usajili.

Pogba katika kipindi hiki cha usajili.
No comments:
Post a Comment