LONDON,
England
KIPA wa Chelsea,
Thibaut Courtois, ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Real Madrid, hajaripoti
katika mazoezi ya timu hiyo ya Ligi Kuu ya England juzi.
Inaelezwa
kuwa, the Blues hadi sasa hawajui lini kipa huyo wakimataifa wa Ubelgiji mwenye
umri wa miaka 26, atarudi kundini katika kikosi hicho cha Chelsea.
Courtois amekuwa
mchezaji wa Blues tangu mwaka 2011, wakati aliposajiliwa kutoka klabu ya
Ubelgiji ya Genk na alichukuliwa kwa mkopo na Atletico Madrid.
Winga wa Chelsea,
Eden Hazard naye pia amekuwa akihusishwa na Real, lakini Jumatatu hakuhudhuria mazoezi
na klabu hiyo.
Courtois alitajwa
kuwa kipa bora katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Urusi mwaka huu,
ambako Ubelgiji iliifunga England katika mchezo wa kusaka mshindi watatu.
Ameichezea
Chelsea mechi 154, akicheza mara 58 bila kufungwa.
Akizungumza
juzi, kocha mpya wa Blues Maurizio Sarri alisema hana uhakika kama Courtois ataendelea
kuwepo katika klabu hiyo.
Alisema:
"Kwa sasa Courtois ni kipa wa Chelsea. Sijui huko mbele. Itategemea na
klabu, hasa itamtegemea yeye mwenyewe ana msimamo gani na anataka nini, lakini
ninategemea Courtois ataendelea kuwa kipa wetu.”
Taarifa
zingine zinasema kuwa, Chelsea wako tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 89 ili
kumnasa kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak kama mbadala wa Thibaut Courtois
kama kipa huyo ataondoka kwenda Real Madrid.
No comments:
Post a Comment