1. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (mwenye suti nyeusi) hivi
karibuni akiongea na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane
alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
Na
Mwandishi Wetu, Simiyu
SHIRIKA
la Mawasiliano nchini (TTCL), limeahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali mwakani,
ili fedha hizo zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu
ya viwanja vya ndege vya serikali.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba ambaye alitembelea banda la
maonesho ya Kilimo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika
kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, amesema wingi huo wa fedha utatokana
na mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa kutumia huduma mbalimbali
zinazotolewa na shirika hilo.
1. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akipata maelezo mbalimbali kutoka
kwa Ofisa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Edward Kimaro alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane
la Mamlaka, yanafanyika kwenye Uwanja wa Nyakabidni mkoani Simiyu.
“Mwaka
huu tulitoa gawio la sh. Bil 5.1 kwa serikali, lakini ninaimani mwakani tutatoa
zaidi endapo tutapata ushirikiano wa kutumiwa kwa huduma zetu kutoka kwenye
taasisi nyingine za serikali, ambapo fedha hizo zinasambazwa na serikali kwenye
kazi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa viwanja vya ndege,” amesema Bw. Kindamba.
Bw.
Kindamba ameishukuru TAA kwa kuanza kutumia huduma ya mawasiliano ya simu kutoka
kwenye shirika hilo, ambapo itasaidia kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi.
Amesema
anaahidi kuimarisha ushirikiano na TAA, na wapo tayari kutumia huduma zinazotolewa
na mamlaka kwa maslahi ya nchini, ili kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi.
1.
Baadhi ya wanakamati ya maonesho ya
Kilimo na sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Tanzania (TAA), wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)
(mwenye suti).
“Ushirikiano
wetu utasaidia kuongeza mapato, ambapo kila taasisi moja itaweza kutumia huduma
na bidhaa za taasisi nyingine, kwa lengo la kuzifanya ziendelee kukua na
kuimarika kiuchumi, kwani taasisi za umma zinategemeana zenyewe kwa zenyewe,”
amesema.
Pia
ameipongeza TAA kwa jitihada zake za kujitangaza kwa wananchi, ambapo ameitaka
kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege.
“Nawapongeza
kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujitangaza, naomba muendelee kuboresha viwanja
vya ndege kwa maslahi ya Watanzania wote, kwa kweli najivunia sana uwepo wenu
katika Nanenane “I am proud of your success’ na kweli mna iunganisha Tanzania
kwa Ulimwengu,” amesema Bw. Kindamba.
1.
Raia wa China wanaofundisha kwenye shule
ya ya sekondari ya J.W.Bukanga Musoma, Bi. Jane Lee (wapili kushoto) na Bi. Cary Zhang (watatu kushoto) wakimsikiliza
Afisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Bakari Mwalwisi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu vimiminika kwenye banda la
maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye
Uwanja wa Nyakabindi, mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment