ZURICH, Uswisi
MANCHESTER United itaungana na Cristiano Ronaldo baada
ya kupangwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A, Juventus katika hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Ronaldo, ambaye aliichezea Man United kwa mafanikio
makubwa katika miaka ya 2003 na 2009, alijiunga na Juve kwa gharama ya pauni
milioni 99.2 mwezi uliopita baada ya miaka tisa ya kuitumikia Real Madrid.
Valencia na Young Boys ni timu zingine zilizopangwa
katika Kundi H.
Tottenham wenyewe wamepnagwa katika kundi gumu,
ambapo itawabidi kukabiliana na wakali Barcelona, wakati washindi wa pili wa
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu huu, Liverpool watakabiliana na Paris
St-Germain (PSG) na Napoli.
Mabingwa PSV Eindhoven na Inter Milan wanakamilisha
Kundi B, ambalo pia litakuwa na timu ya England Tottenham na Red Star Belgrade ni
timu nyigine ambayo itacheza na kikosi cha kocha Jurgen Klopp katika Kundi C.
Mabingwa wa Ligi ya England Manchester City wamepangwa
katika Kundi F pamoja na Shakhtar Donetsk, Lyon na Hoffenheim.
Mabingwa watetezi Real Madrid, ambao wameshinda taji
hilo kwa miaka mitatu mfululizo, wenyewe wako katika Kundi G pamoja na Roma,
CSKA Moscow na Viktoria Plzen.
Ratiba
Kamili ya Makundi:
Kundi A: Atletico Madrid, Borussia Dortmund, Monaco
na Club Brugge.
Kundi B: Barcelona, Tottenham, PSV Eindhoven na Inter
Milan.
Kundi C: Paris St-Germain, Napoli, Liverpool na Red
Star Belgrade.
Kundi D: Lokomotiv Moscow, Porto, Schalke na Galatasaray.
Kundi E: Bayern Munich, Benfica, Ajax na AEK Athens.
Kundi F: Manchester City, Shakhtar Donetsk, Lyon na Hoffenheim.
Kundi G: Real Madrid, Roma, CSKA Moscow na Viktoria
Plzen.
Kundi H: Juventus, Manchester United, Valencia na Young
Boys.
No comments:
Post a Comment