Mwandishi Wetu,
Tabora
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe
Magufuli ameagiza ujenzi wa mradi wa jengo
la abiria 500 kwenye Kiwanja cha Ndege cha Tabora uanze mara moja.
Rais ametoa kauli
hiyo mara baada ya kufungua ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa
miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Tabora, ambapo alisema sasa abiria
wataongezeka kutokana na kukamilika kwa ujenzi huo, hivyo italazimu jengo kubwa
lenye kuchukua abiria 500 kwani la sasa lenye uwezo wa kuchukua abiria 50
halitatosha.
“Ninaimani kubwa kwa
ujenzi huu lazima idadi ya abiria itaongezeka zaidi, hivyo kwa hili jengo dogo
halitatosheleza abiria watakaoongezeka hivyo, namuagiza Waziri (Makame Mbarawa)
kuanza mchakato wa ujenzi wa jengo hilo kubwa, ,” alisisitiza Rais Magufuli.
Amesema kutokana na
ukarabati na upanuzi huo sasa kiwanja hicho kitaruhusu kutua kwa ndege kubwa
zaidi za ndani na nje ya nchi, na kufanya wakazi wa mkoa wa Tabora kutumia
uisafiri wa ndani kwa kwenda Dar es Salaam, Burundi, Kenya, Rwanda na maeneo
mengine.
Amesema anarajia
ujenzi huo utakamilika mapema zaidi na atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa
jengo hilo, ambapo aliwapongeza Wizara pamoja na wafanyakazi wote wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Rais amesema
serikali yake inataka maendeleo ya kuwa na viwanja vya ndege vya uhakika,
barabara na maji na sio siasa, ambazo hazina tija kwa maisha ya wananchi sasa
na baadae.
“Mimi ni Rais wa Watanzania wote na sio wa CCM
pekee na ndio maana ninachochea maendeleo tena ya haraka ambayo yatafanikisha
wananchi kuwa na maisha mazuri ikiwa ni pamoja na kuitumia miundombinu katika
biashara na maisha yao ya kila siku,” amesema Rais.
Katika hatua
nyingine, Rais ametaka barabara ya kutua na kuruka kwa ndege irefushwe zaidi
ili kuruhusu ndege kubwa kutua kwa wingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu mbalimbali ya Kiwanja cha ndege cha Tabora. |
Naye Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amesema sambamba na
maboresho hayo ya miundombinu katika kiwanja cha ndege cha Tabora, sasa ujenzi
wa jengo jipya la abiria unatarajia kuanza mara moja kwa ufadhili wa fedha za
mkopo kutoka Benki ya Uwekezaji ya Uaya (European Investment Bank-EIB), na
litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka.
Pia Mbarawa amesema
mradi huu wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha
Tabora umegharamiwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Mbarawa amesema
mradi huu umejumuisha barabara za kuruka na kutua ndege, barabara ya kiungio,
maegesho ya ndege, taa na mitambo ya kiusalama ya kuongoza ndege wakati wowote
na kituo cha umeme.
“Kiwanja sasa
kimeongezewa uwezo wa kutoa huduma kwa saa 24, na vilevile maboresho
yanayofanyika katika viwanja viwanja vya ndege yanalengo la kuvutia ujaji wa
mashirika mengi zaidi ya ndege pamoa na kuongeza uwezo wa kuhudumia ndege
nyingi zaidi, na sasa serikali inadhamiria ya kununua ndege nne na jum;a
itafanya idadi ya ndege sita,” amesema Mbarawa.
Naye Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kiwanja cha Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi
amesema ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja cha ndege cha Tabora
umefanyika kwa awamu tatu, ambapo ni kujenga barabara ya kwanza ya kuruka na
kutua kwa ndege kwa kiwango cha lami kwa urefu wa mita 1900 na upana wa mita 30.
Msangi amesema awamu
ya pili ilihusisha ujenzi wa barabara ya pili ya kuruka na kutua kwa ndege kwa
kiwango cha lami yenye urefu wa mita 1260 na upana wa mita 23; maegesho ya
ndege yenye uwezo wa kuegesha ndege tatu zenye ukubwa wa ATR 72 au Bombardier
dash 8 Q400 kwa wakati mmoja; kujenga kiungio yenye urefu wa mita 250;
usimikaji wa taa na mitambo ya kuongezea ndege wakati wa kutua na kuruka.
“Hii awamu ya pili
ilihusisha vitu vingi ikiwepo pia ujenzi wa kituo cha kufua umeme na usimikaji
wa jenereta lenye kVA 500; ujenzi wa uzio wa usalama wa urefuwa kilometa 2.6 na
ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua,” amesema Msangi.
No comments:
Post a Comment