Na Mwandishi Wetu, kibaha
SERIKALI imesema Tanzania inatakiwa kuanza mapema maandalizi ili kupata medali katika mashindano mbalimbali yajayo ya kimataifa.
SERIKALI imesema Tanzania inatakiwa kuanza mapema maandalizi ili kupata medali katika mashindano mbalimbali yajayo ya kimataifa.
Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrson Mwakyembe wakati akifungua mafunzo ya siku
13 ya makocha wa riadha ya hatua ya kwanza ya wachezaji wenye umri chini ya
miaka 16 katika Kituo cha Michezo cha Filbert Bayi Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura. |
Tanzania inatarajia kushiriki Michezo ya
Jumuiya ya Madola itakayofanyika Gold Coast, Australia 2018, ile ya Mataifa ya
Afrika 2019 na Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) akizunguza wakati wa mafunzo hayo. |
Dk Mwakyembe alisema kuwa Tanzania inaweza
kufanya maajabu katika mashindano ya kimataifa kutokana na vipaji vilivyopo
katika michezo mbalimbali kama wachezaji wataandaliwa vizuri na mapema.
Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau (kulia) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura. Kulia kwa Waziri ni Makamu wa Pili wa Rais Riadha Tanzania (RT), Dk Hamad Ndee. |
"Tuna mashindano makubwa mbele yetu,
kama Jumuiya ya Madola 2018 Australia, Michezo ya Afrika 2019 Guinea ya Ikweta
na ile ya Olimpiki mwaka 2020. “ alisema.
"Sasa tunatakiwa kuangalia mbele
maandalizi ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,
“alisema.
Mwakyembe alisema alibaini vipaji katika
mashindano ya vijana ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 18 ya riadha
iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati
wanariadha chipukizi walipoonesha uwezo
wa hali ya juu.
Pia aliitaka Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) kuratibu vizuri kozi hiyo kwa kushirikiana na vyama vya michezo vya
Tanzania (RT) na kile cha Zanzibar (ZAAA) chini ya udhamini wa Mshikamano wa
Olimpiki ((OS).
Akizunumza mapewa mmoja wa wakufunzi wa
mafunzo hayo kutoka Uganda, Charles Mukiibi
alisema mafunzo hayo yanaleng katika kutoa ujuzi wa kufundisha watoto
wenye umri chini ya miaka 16 na chini yake, wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa
shule za msingi, ambao wanalenga kuwa mabingwa wa baadae.
Makamu wa Rais wa Riadha Tanzania (RT), Dk
Hamad Ndee alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani yatasaidia
kuongeza idadi ya makocha wa mchezo huo hapa nchini.
"Tunaishukuru TOC kwa jitihada kubwa
walizofanya hadi kutupatia mafunzo haya, ambayo yatatusaidia kuuendeleza mchezo
huu hapa nchini, “alisema Katibu Mkuu wa ZAAA, Suleiman Ame wakati akitoa
salama za shukrani kwa niaba ya washiriki wote.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia mikoa
kutoa wanariadha wengi chikupukizi ambao watafanya vizuri siku za usoni.
Naye katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema
kozi hiyo imeratbiwa na RT na ZAAA pamoja na TOC.
Bayi,ambaye ni gwiji wa zamani wa riadha
Tanzania alisema kuwa vyana vya riadha vya mikoa haviko hai kutokana na ukosefu
wa wanariadha chipukizi, ambao vipaji vyao haviendelezwi.
Alisema tayari TOC imeshatoa kozi 19 kwa
viongozi wa vyama vya michezo vya kitaifa na makocha katika harakati za kuendeleza michezo nchini.
Alisema ni jukumu la vyama vya michezo
kuhakikisha mafunzo hayo yaliayoanza mwaka 2005, yatoa matunda.
Alisema kuwa TOC imekuwa ikifanya kazi bila
kuchoka kuhakikisha Tanzania inatoa wakimbiaji watakaofanya vizuri katika
mashindano mbalimbali.
Alisema kuwa Tanzania inahitaji wanariadha chipukizi ikiwa nchi
iliyopo katika 10 bora zilizoshiriki katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika
Rio de Janeiro 2016.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni
rasmi, Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau alisema ufinyu wa program za
maendeleo kwa vyama vya michezo, masoko na udhamini ni miongoni mwa viti
vinavyorudisha nyuma maendeleo ya michezo hapa nchini.
Vyama vya michezo vinatakiwa kuwa na program
za uhakika na kuelekeza maandalizi yao katika mashindano makubwa badala ya
kusubiri muda umekwisha ndio wafanye maandalizi ya zima moto.
No comments:
Post a Comment