Monday, 31 July 2017

Timu ya Taifa ya Riadha yaagwa, waahidi medali

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimkabidhi bendera ya taifa nahodha wa timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya dunia London, Uingereza, Felix Simbu leo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Saalm. Kulia ni Rais wa RT, Anthony Mtaka na kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Multichoice, Maharage chande.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano ya riadha ya Dunia yanayoanza wiki hii London, Uingereza imeagwa leo kwa  kukabidhiwa bendera ya taifa jijini Dar es Salaam ikiwa nishara ya kuwa wawakilishi maalum wa nchi yetu katika mashindano hayo makubwa.

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe aliyekabidhi bendera kwa nahodha wa timu hiyo, Felix Simbu.
Timu hiyo itaondoka afajiri ya kuamkia kesho ikiwa na wachezaji nane, makocha wawili na viongozi wawili, huku Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday akitangulia kuhudhuria vikao mbalimbali akimwakilisha Rais wa RT Anthon Mtaka.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa wizara yake iko bega kwa began a wadau wa michezo haa nchini kuhakikisha kuwa kuwa tunaiga hatua katika sekta hiyo na kuifanya kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato kwa wanamichezo wetu.
Amesema Serikali imejizatiti kikamili katika kuratibu na kurasimilisha michezo haa nchini ili wanamichezo watambue kuwa hiyo ni kazi tena ya heshima kubwa na yenye malio makubwa.

Waziri Mwakyembe ia alionesha kuridhika na viwango vya wachezaji na  kueleza imani yake kubwa kuwa wataweza kutuletea medali.
Waziri ameioneza Kamuni ya Multichoice-Tanzania kwa udhamini wake mkubwa katika maandali ya timu hiyo, ambao kamuni hiyo ilikuwa mdau mkubwa kufanikisha mafunzo katika kambi hiyo.

Naye Rais wa Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka, amesema mbali na jitihada kubwa zinazofanywa na chama hicho, bado zipo changamoto nyingi, ambazo zinahitaji nguvu za pamoja ili kuhakikisha kuwa riadha inasonga mbele.
Kwa uande wake Mkurugenzi wa Multichoice, Maharage Chande amesema kuwa kampuni yake ina dhamira endelevu ya kuinua na kuibua vipaji hapa nchini  na ndiyo maana wakaamua kusaidia katika maandalizi ya timu.

Akizungumza baada ya timu hiyo kukabidhiwa bendera, mmoja wa wanariadha hao, Simbu alisema kuwa wao wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanarudi nchini na medali baada ya wanariadha wa Tanzaniua kusindwa kuipata kwa zaidi ya miaka 10.
Kwa mara ya mwisho Tanzania ilitwaa media kutoka katika mashindano ya dunia mwaka 2005 yaliyofanyikia Helsinki, Finland wakati Christopher Isegwe aliotwaa medali ya fedha.

Mbali na Simbu wanariadha wengine wa marathon waliomo katika timu hiyo ni Saida Makula, Stephano Huche, Magdalena Shauri pamoja na Sarah Ramadhani wakati mbio za meta 5,000 watashiriki akina Gabriel Geay na Emmaniel Giniki huku Failuna Abdul atashiriki mbio za meta 10,000.
 




 

No comments:

Post a Comment