Mratibu wa mbio za Kilifm Marathon, Nelson Mrashani akizungumza kuhusu mbio hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. |
KAMPUNI zimezidi
kujitokeza kufanikisha mbio za pili za Kilifm Marathon zitakazofanyika Agosti
13 mjini Moshi.
Mratibu wa mbio hizo
Nelson Mrashani akizungumza kwa njia ya simu jana alisema maandalizi yanaenda
vizuri na wamepata wadhamini.
Mrashani aliwataja
wadhamini hao kuwa ni pamoja na Wiva Entertaiment, Mr UK, Maji ya Kilimanjaro,
Kampuni ya Coca Cola, Radio Kilfm, Temeck Car Tracking, Tanzania Media
Foundation, Finca Bank na Ciascom Tech Engeeniring.
Alisema kuwa tayari
usajili wa mbio hizo umeanza, ambapo mwaka huu wanatarajia kupata washiriki
zaidi ya 3,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Mbio hizo
aitahusisha umbali wa kilometa 21, kilometa tano , ambazo zitawashirikisha
wafanyakazi wa taasisi mbalimbali pamoja na watu wazima wakati zile za kilometa
2.5 zitakuwa na watoto wadogo.
Zawadi za washindi
zitakuwa za aina tofauti, ambapo washiriki wa kilometa 21 wenye umri wa miaka
45-60 na hadi 100 watapewa zawadi maaluma wakati wakibiaji wakawaida watakuwa
na kundi lao.
Pia washindi watatu
watatu wa mbio zote watapata fursa ya kwenda kutembelea hifadhi ya Ngorongoro
ili kuhamasisha utalii wa ndani kupitia Kituo cha Kilifm Sport Centre.
No comments:
Post a Comment