Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
Salum Mayanga amesema kuwa timu yake imeshindwa kuibuka na ushindi katika
mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (Chan) kwa wachezaji wa
nyumbani baada ya kufungwa bao la mapema na Rwanda kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
hapa.
Taifa Stars ilifungwa bao katika dakika ya 17 na kuwa
na kibarua cha kutafuta bao la kusawazisha, ambalo walilipata kwa penalti.
Mayanga aliyasema hayo baada ya mchezo huo was are ya
kufungana bao 1-1 na timu yake kujiweka katika nafasingumu ya kusonga mbele
katika mashindano hayo. Bao la wageni lilipachikwa na Dominique Nshuti.
Kukosa utulivu ni jambo jingine ambalo limechangia Taifa
Stars kushindwa kupata matokeo ya ushindi. Mayanga alisema kuwa wapinzani wao walitumia
mbinu ya kupoteza muda ili kupata matokeo ya sare.
Naye kocha wa Rwanda alisema kuwa wanajipanga kqa
ajili ya mchezo wa marudiano kwani mchezo huo bado haujamalizika lakini alisema
timu ya Tanzania sio timu ya kuibeza kwani iko vizuri.
Matokeo hayo yanamaanisha Taifa Stars italazimika
kwenda kushinda ugenini mjini Kigali Julai 22 ili kusonga mbele katika kuwania
tiketi ya CHAN mwakani nchini Kenya, ambako itamenyana na mshindi kati ya Sudan
Kusini na Uganda zilizotoa sare ya 0-0 pia jana mjini Juba.
No comments:
Post a Comment