Na Mwandishi Wetu
KAMA ilivyo ada, King’amuzi cha DStv kitaonyesha mubashara
mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Tanzania na Zambia ikiwa ni nusu
fainali ya michuano ya COSAFA 2017 itakayochezwa kesho Jumatano saa 12 jioni
huko Afrika Kusini
Taifa stars imefuzu nusu fainali baada ya shughuli pevu ya
kuwafunga wenyeji Africa Kusini (Bafana Bafana) na sasa itakumbana na moja ya
miamba ya soka barani Afrika Zambia katika nusu fainali inayotarajiwa kuwa na
upinzania mkali.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria
amethibitisha kuwa mechi hiyo itarushwa mubashara kupitia DStv chaneli ya
SuperSport4 ambayo inapatikana kwenye vifurushi vyote kikiwemo kile cha DStv
Bomba ambacho hupatikana kwa Sh 19,975 tu.
“Kwanza kabisa tunawapongeza sana Taifa Stars, wamefanya kazi
kubwa, wameleta matumaini makubwa, sasa kazi ni moja tu, kwenda fainiali na
sisi DStv, tunawahakikishia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa mtanange
huo watauona mubashara kupitia DStv” alisema Alpha.
Ameongeza kuwa enzi ya watanzania kusubiri matokeo ya
michuano mikubwa kama hii ka saa kadhaa baada ya mechi kukamilika umepitwa na
wakati, kwani kwa DStv, michuano hiyo huonyeshwa moja kwa moj. “Hakuna tena
kwend amtandaoni kuangalia matokeo, wala kumuuliza mtu, ukiwa na DStv,
unashuhudia mwenyewe” alisema.
Huduma za DStv zimekuwepo hapa Tanzania kwa miaka 20 sasa na
maelfu kwa maelfu ya watanzania wameunganishiwa huduma za DStv na kuwafanya
mamilioni ya watanzania katika kila pembe ya nchi kufurahia huduma zake. Mbali
na kujikita Zaidi katika michezo na burudani, DStv pia ina chaneli mbalimbali
za habari, Sanaa, Dini, Utafiri, Sayansi na Teknolojia, na pia utamaduni.
No comments:
Post a Comment