MBIO kubwa zaidi za marathoni zinatarajia kufanyika
Moshi Novemba 19 mwaka huu, ambazo zitajulikana kama Kilimanjaro International
Airport Marathoni, imeelezwa.
Mbali na kutarajia kushirikisha wanariadha wengi tena
nyota kutoka ndani nan je ya Tanzania, mbio hizo zitakuwa zinaongoza kwa zawadi
kubwa, ambao mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha sh milioni 7 ikiwa ni
zawadi kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika mbio za marathon hapa nchini.
Mkurugenzi wa Mbio hizo, Amini Kimaro akizungumza leo jijini Dar es Salaam. |
Kimaro alisema kuwa mshndi wa pili wa mbio hizo za
kilometa 42 ataondoka na kitita cha sh milioni 5 huku watatu atakabidhiwa
kitita cha sh milioni 4 wakati mshindi wanne atapewa sh milioni 2.5 huku yule
watano atabeba sh milioni 2.
Alisema kuwa zawadi za washindi watazitoa hadi kwa
mshindi wa 10, ambaye ataondoka na kitita cha sh 500,000.
Mkurugenzi msaidizi wa mbio, Kunda Ndosi. |
Kwa upande wa mbio za nusu marathon au kilometa 21,
zile za Kilimanjaro International Airort wenyewe mshindi wa kwanza ataondoka na
kitita cha sh milioni 4 wakati Kilimanjaro Marathon wanatoa sh milioni 2 tu.
Mbio za Kilimanjaro International Airport zitatoa zawadi
za fedha taslimu hata kwa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za kilometa tano,
mbio za Kilimanjaro Marathon zenyewe hutoa zawadi za saa na vitu vingine
vinavyotolewa na wadhamini wa mbio hizo za kilometa tano.
Hakuna ubishi kuwa zawadi za washindi wa mbio hizo ni
nono kweli ukilinganisha na zingine zote zinazofanyika hapa nchini katika
vipindi tofauti tofauti vya mwaka.
Mbali na ukubwa wa mbio hizo, pia zitakuwa ni za
kipekee kwani zitaanzia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) na kumalizikia katika maeneo hayo hayo.
Mbio hizi zitajumuisha zile za full marathon, yaani
kilometa 42, nusu marathon yaani za kilometa 21 na zile za kilometa tano,
ambazo wengine wanaziita mbio za kujifurahisha na hazina zawadi.
Hatahivyo, waandaaji wa mbio hizo za kimataifa za
Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro, wenyewe watatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza
hadi watano, ambao watapata sh 500,000, 300,000, 250,000, 225,000 na 200,000.
Kimaro anasema kuwa wameamua kutoa zawadi nono ili
kuvuta nyota wengi wa riadha hapa nchini na nje ya mipaka yetu ili kuzifanya
ziwe kubwa zaidi.
Anasema kuna viwanja kadhaa vya ndege duniani
vimekuwa vikiandaa mbio ili kuvuta watalii na watu wengine kama vile Dubai
Marathon na Helsink nchini Finland.
Anasema mshindi wa pili ataondoka na kitita cha sh
milioni 5, wakati wa tatu atapewa sh milioni 4, huku yule wa nne atapewa sh milioni 2.5, watano
sh milioni 2 na wa sita sh milioni 1.
Mshindi wa saba ataondoka na sh 800,000 wakati yule
wa tisa atapata 700,000 wa tisa na 10 atapata sh 600,000 na 500,000.
MBIO MPYA ZA WANAFUNZI
Hii ni mara ya kwanza kwa waandaaji wa mbio
kuwakumbuka wanafunzi, ambapo kutakuwa na mbio maalum za wanafunzi za kilometa
21, ambapo wanafunzi watatumia fedha za ushindi kulipia ada zao.
Mbali na kuwashindanisha wanafunzi, pia mbio hizo za
nusu marathoni zitashirikisha wanariadha wa kawaida ambao nao watakuwa na
zawadi zao.
Zwaadi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambao
watashindana katika kilometa 21 zikuwa ni sh milioni 4 kwa mshindi wa kwanza
wakati mshindi wa pili ataondoka sh milioni 3 wakati mshindi wa tatu atapata
milioni 2.5.
Kimaro ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Riadha
Wilaya ya Hai na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Mkoa wa
Kilimanjaro alisema wanafunzi watatumia fedha hizo kwa ajili ya kulipia ada ya
vyuo.
“Mbio za nusu marathoni ziko pande mbili, upande
mmoja zinashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu ambao zawadi hizo za washindi
zitawawezesha kulipia ada zao za vyuo, “alisema Kimaro.
NAOMBA KUFAHAMU UTARATIBU WA KUJIUNGA UPOJE
ReplyDeletejumatatu ndo utaratibu unaanza
Deletethat is so wanderfull i will be there
ReplyDelete