Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya mbio za nne
za Kihistoria za Bagamoyo zitakazofanyika Jumapili, Agosti 6, mjini humo, yamepamba moto.
Mratibu wa mbio hizo,
Dominic Mosha alisema jana kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wanatarajia
zaidi ya wanariadha 500 kushiriki mbio hizo mwaka huu.
Alisema mbali na mbio kuu
za kilometa 21, pia kutakuwa na mbio za kilometa 10 na zile za kujifurahisha za
kilometa tano ambazo hazina zawadi lakini kila mshiriki atapata fulana.
Alisema washindi watatu
wa kwanza wa mbio za kilometa 10 kila mmoja ataondoka na medali.
Alisema mbio za mwaka huu
zitakuwa na msisimko wa aina yake na zitaandaliwa kwa ubora zaidi, kwani kila
mwaka wanapata uzoefu zaidi wa kuandaa kitu bora.
Mosha aliwataka washiriki
kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo, ambazo ni maalum kwa ajili ya kutangaza
mji wa kihistoria wa Bagamoyo.
Alisema kuanzia leo
wanatarajia kuweka vituo vya usajili wa shiriki ili kuwawezesha wengine ambao
hawajaweza kujisajili katika mtandao kufanya hivyo.
Mbio hizo hufanyika kila
mwaka na kuandaliwa na 4Bell, ambapo lengo ni kuibua na kuendeleza vipaji
pamoja na utalii mjini Bagamoyo na vitongoji vyake.
Mwaka jana mbio hizo
zilifanyika Julai 24 na kushirikisha washiriki kibao kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania.
No comments:
Post a Comment