MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amebwaga
manyanga kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.
BBC Sport ilirioti Juni kuea Ronaldo alikuwa
tayari kuondoka baada ya kutuhumiwa kukwea kulipa kodi na anataka kuondoka
Hispania.
Kurejea Man United, ambako aliondoka wakati
huo kwa ada iliyokjwa rekodi ya dunia ya pauni milioni 80 mwaka 2009, ilitajwa
kama moja ya sehemu anayoweza kutua.
Hatahivyo, alioulizwa kuhusu uwezekano wa
mchezaji huyo kurejea Man United, Mourinho alisema hilo haliwezi kutokea
kutokana na ugumu wa kiuchumi wa kukamilisha uhamisho huo.
Mourinho alipoulizwa kumsajili nahodha wa
Ureno Ronaldo Ronaldo baada ya timu yake kuifunga LA Galaxy 5-2 katika mchezo
wa kwanza wa maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mpya katika ziara ya Marekani
leo Jumapili.
"Kamwe siwezi kuruhusu klabu yangu
kupoteza muda kwa kitu ambacho hakiwezekani.
"Ronaldo ni mchezaji mzuri kwa klabu
yake. Hatuna sababu ya kutufanya kufikiria kama Ronaldo kama anaweza kuondoka.”
Mourinho aliongeza kuwa aamini kuwa hakuna
mchezaji mwingine wa Real Madrid, mshambulia Alvaro Morata, huenda akaishia Old
Trafford.
"Ni aibu, " alisema.
No comments:
Post a Comment