Na Mwandishi Wetu
KIFIMBO cha Malkia wa Uingereza kimetua jijini Dar es
Salaam leo huku wanafunzi wa shule ya Msini ya Filbert Bayi waking'ara na ngoma yao ya Mganda wakati wa kukipokea kifimbo hicho kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).
Kifimbo hich kesho kitakimbizwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Ikulu, ambako litapokewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan.
Wanafunzi hao wa shule ya Filbert Bayi walikonganyoyo za wakimbiza kifimbo hicho pamoja na wageni waalikwa waliofika uwanjani hapo kukipokea, ambapo walichenua kwa `atep zao bila kukosea, mbali na mavazi yao meupe na vitambaa vyekundu vichwani mwao.
Ndege ya Kenya Airways ndiyo iliyokibeba Kifimbo
hicho kutoka Kenya na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) na watu mbalimbali wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Coke na Balozi wa Australia nchini
Kenya, John Feakes.
Kifimbo hicho kilipotua nchini kilibebwa na Makamu wa
Rais wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola Afrika, Gideon Sam pamoja na
Rais wa TOC, Gulam Rashid na kuingia nacho katika jengo la kuwasilia na
kuondokea abiria maarufu la VIP la JNIA.
Katibu Mkuu wa
TOC, Filbert Bayi akizungumza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius
Nyerere (JNIA) leo. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Coke na Rais
wa TOC, Gulan Rashid.
|
Akizungumza uwanjani hapo Sam alisema kuwa kifimbo
hicho ni ishara ya kukaribia kufanyika kwa Michezo ya 21 ya Jumuiya ya Madola
itakayofanyika Gold Coast, Australia Aprili mwakani.
Alisema kifimbo hicho kimetokea Kenya, ambao walikipokea
kutoka nchini Nigeria.
Naye Feakes
alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuelimisha kuhusu kifimbo
hicho, ambacho kinakimbizwa kila kabla ya michezo inayokuja ya Jumuiya ya
Madola.
Rais wa TOC, Rashid alisema wanafurahi kukipokea
kifimbo hicho , ambapo kesho watakikimbiza hadi Ikulu.
Bayi akitaja ratiba ya kifimbo hicho kesho asubuhi
kitaanzia Azam TV kabla ya kwenda katika daraja la Nyerere na baadae kwenye
Uwanja wa Taifa, ambako kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za burudani
kutoka African Stars `Twanga Pepeta’, JKT, Polisi na vikundi vingine, kabla ya
kuanza mbio kwenda Ikulu.
Kifimbo hicho jioni kitakwenda Arusha katika shule ya
St Judy na baadae kurudi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment