Wachezaji wa timu ya Uchukuzi Sports Club wa timu ya Kuvuta Kamba wakijifua kwa ajili ya mashindano ya Mei Mosi. |
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Uchukuzi Sports imetamba kutetea mataji yake na kuongeza mengine
katika mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika kuanzia wiki ijayo mjini Moshi.
Katibu wa Michezo wa Uchukuzi Sports Club, Alex Temba alisema juzi wakati
wa mazoezi ya timu hiyo kuwa, wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanatetea mataji
waliyonayo na kuongeza mengine.
Timu ya soka ya Uchukuzi wakati wa mapumziko walipocheza jana dhidi ya Kitunda FC na kutoka sare ya bila kufungana. |
Akifafanua, Temba alisema kuwa Uchukuzi Sports ndio mabingwa wa jumla wa
mashindano hayo ya wafanyakazi, ambao waliutwaa mwaka jana mjini Dodoma na
kukabidhia Kombe na Rais Dk John Pombe Magufuli.
Alisema wanakwenda Moshi kutetea mataji ya soka, kuvuta kamba kwa
wanawake na wanaume, mbio ndefu kwa wanaume na wanawake, baiskeli kwa pande
zote mbili pamoja na michezo ya jadi ya bao, karata na drafti.
Timu ya netiboli wakijfua. |
Alisema kuwa maandalizi yao ambayo walianza muda mrefu, yanaendelea
vizuri na wanatarajia kuondoka wiki ijayo kwenda Moshi tayari kwa mashindano
hayo.
Timu ya Uchukuzi Sports inaundwa na wachezaji kutoka taasisi zilizochini
ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Naye nahodha wa timu hiyo, Toba Ally alisema kuwa hawana wasiwasi, kwani
wana uhakika maandalizi yao mazuri kuwanyoa wapinzani wao katika michezo yote.
Alisema mwaka jana walitwaa vikombe vitano, lakini mwaka huu watabeba
mataji zaidi, kwani maandalizi yao ndio yanawafanya kujiamini kiasi hicho.
No comments:
Post a Comment