Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande (kulia), Alphonce Simbu (katikati) na kocha wa Simbu, Francis John. |
Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa Medali ya Dhahabu katika Mbio za Mumbai, Alphonce Simbu
amewasilili katika jiji la London tayari kwa kushiriki London
Marathon yanayofanyika jijini keshokutwa Jumapili.
Simbu amewasili nchini Uingereza tayari kwa mashindano hayo ambayo
yanayotarajiwa kushirikisha wanariadha mashuhuri duniani.
Simbu, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika
mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kuwapa
wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizo za London
akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele pamoja na wengine kutoka Ethiopia na Kenya.
Akiongea muda mfupi kabla ya kupanda Ndege kwenda Uingereza, Simbu
alisema amejiandaa kupambana kufa na kupona kuhakikisha kuwa ananyakua medali
kwenye mashindano hayo.
“Nitapambana kwa nguvu zangu zote. Ninakwenda London nikijua wazi kuwa
naiwakilisha nchi yangu kwenye mashindano haya makubwa. Nakwenda kupeperusha
bendera ya Tanzania” alisema simbu
Aliongeza kuwa “Nina imani nitashinda kwani nimefanya mazoezi ya kutosha
na nina ari na moyo wa kushinda. Naomba sala za watanzania wote ili niweze
kuleta medali nyumbani” Alisema Simbu.
Simbu kwa sasa yu[o chini ya udhamini wa kampuni ya Multichoice Tanzania
kupitia King’amuzi cha DStv ambao ndio wamedhamini kambi yake.
“Nawashukuru sana DStv kwa
udhamini wao mkubwa wa kambi yangu ya mazoezi pamoja na mahitaji yangu mengine
kwa kipindi kirefu sasa. Kwa kweli wao ndiyo waliofanikisha maandalizi yangu”
alisema Simbu
Mbali na wadhamini pia amewashukuru wadau wote wa riadha hususan Chama
Cha Riadha Tanzania pamoja na wizara inayohusika na michezo kwa jitihada zao za
kuahakikisha safari yake ya kwenda London inafanikiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema kuwa
wana imani kubwa sana na Simbu kutokana na mazoezi aliyofanya.
“Tunafurahi sana kuwa baada ya kuweka nguvu kubwa sasa Simbu anakwenda
kushiriki mashindano haya akiwa amejiandaa vizuri. Tunaamini atashinda, na pia
huu ni mwanzo wa ndoto yetu kubwa, ya kusikia kwa mara ya kwanza wimbo wetu wa
Taifa ukipigwa kwenye mashindano ya Olympic. Kwa mwenendo wake, tunaamin Simbu
atatufikisha huko” alisema Maharage.
Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo
la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki katika mashindano ya Dunia
yatakayofanyika jijini London Agosti mwaka huu. Udhamini huu ulianza
tangu mwaka 2016, ambapo Multichoice humpatia Alphonce posho ya kujikimu pamoja
na kusaidia kambi yake ya mazoezi.
Alphonce anatarajiwa kurejea nchini Jumatatu, Aprili 24 saa
mbili asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment