Na Mwandishi Wetu
MWANARIADHA wa kimataifa wa Tanzania, Alphonce Simbu kesho
Jumatatu atapanda pipa kwenda Afrika Kusini akiwa njiani kwenda Uingereza,
ambako atashiriki London Marathon Jumapili ijayo Aprili 23.
Simbu anapitia Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa viza ya
dharura ya kuingia Uingereza baada ya kuikosa ile ya kawaida jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday
alisema jana kuwa, Simbu ataondoka kesho Jumatatu kwenda Afrika kusini
kushughulikia viza ya kuingia Uingereza kabla ya kwenda nchini humo ambako
Jumapili atashiriki London Marathon.
Simbu alifuzu kwa mbio hizo baada ya kumaliza katika nafasi
ya tano katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika Rio de Janeiro, Brazil 2016
kabla ya kushinda mbio za Mumbai Marathon.
Kwa mujibu wa Gida, tayari mwanariadha huyo ameingia katika
orodha ya wanariadha bora kabisa duniani na ndio maana waandaaji wa London
Marathon kuna fedha atapewa mara tu atakapoanza mbio hizo (Appearance Fees).
Gidabuday alisema kuwa Simbu hata kama hatashinda mbio hizo
lakini akimaliza tu amejihakikishia fungu nono na kama akimaliza, basi
ataondoka na maelfu ya dola za Marekani.
Simbu endapo atashinda mbio hizo za London Marathon
ataondoka na kitita cha dola za Marekani 55,000 kama zaidi yash Milioni 150, na
kama atafanikiwa kuvunja rekodi ataongezewa dola za Marekani 25,000 (ikiwa ni
zaidi ya sh Mil 50),
Mshindi wa kwanza hadi wa 12 wa mbio hizo ataondoka na
kitita cha fedha, huku wale watakaokimbia muda bora bbila kujali kama umevunja
rekodi ya njia au ya dunia, nao wataongezewa fedha za bonasi.
No comments:
Post a Comment