KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali kuhakikisha
inatoa kwa wakati fedha za mradi wa ujenzi wa Mradi wa jengo la tatu la abiria
(TB III) la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ili mradi huo
uweze kukamilika Disemba 2017 kama ilivyopangwa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla alitoa kauli hiyo leo
wakati wa kufanya majumuisho baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi
huo, ambapo ukikamilika jengo hilo litakuwa na uwezo wa kupokeo abiria milioni
6 kwa mwaka.
Prof. Sigalla alisema kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati utapunguza
msongamano wa abiria ambao sasa wanahudumiwa kwenye jengo la pili la abiria la
JNIA (TBII).
uliopangwa utawapa heshima
Watanzania lakini pia kupunguza msongamano katika jengo la sasa la Terminal II.
“Ninawapongeza sana ten asana kwa ujenzi wa jengo hili ikimalizika
ninaimani kubwa litatupa heshima kubwa, hivyo ili likamilike kwa haraka
tunaiomba serikali yetu itoe fedha kwa wakati kwani tumeona ndio moja ya
changamoto zilizozungumziwa hapa,” alisema Prof. Sigalla.
Aliongeza kuwa … “pato la taifa litaongezeka kwa ndege nyingi za nje na
kubwa zitakapokuja kutua kwenye kiwanja chetu,”.
Awali wakati akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo hilo, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim
Msangi alisema, changamoto kubwa inayowakumba ni serikali kuchekewa kutoa
fedha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Prof. Norman
Sigalla akiwaeleza jambo wajumbe wa kamati hiyo, wakati wakitembelea jengo la
tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Bw. Msangi alisema changamoto nyingine ni sheria ya Mamlaka ya Mapato
(TRA) ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ilipitishwa mwaka 2015, awali
kabla ya sheria hiyo kupitishwa vifaa vya ujenzi wa jingo hilo vilikuwa na
msamaha wa kodi, lakini baada ya kupitishwa msamaha huo uliondolewa na
kusababisha baadhi ya vifaa kukaa kwa muda mrefu bandarini baada ya kuzuiwa.
Alisema kutokana na changamoto hiyo ya kuchelewa kwa fedha na vifaa
kukwama bandarini, kumesababisha mradi huo uliokuwa umepangwa awali kumalizika
Agosti 2016 kushindwa kukamilika kwa wakati na sasa unatarajiwa kukamilika
Disemba 2017.
“Tunaiomba serikali itusaidie upatikanaji wa fedha hizi za mradi kwani
hii ni moja ya changamoto kubwa inayotishia kuendelea kwa ujenzi huu,” alisema
Bw. Msangi.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Uchukuzi), Dk Leonard Chamriho alieleza juu ya notisi iliyotolewa na Mhandisi
Mshauri ya kutaka kusitisha huduma kuanzia leo (Jumatano) hadi atakapiliwa
fedha anazodai.
“Tayari serikali imeanza kufanyia kazi deni hili na sasa ipo kwenye hatua
nzuri ya kuhakiki nyaraka za malipo kabla ya kumlipa,” alisema.
IMETOLEWA NA BAHATI MOLLEL, OFISA UHUSIANO MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE
TANZANIA (TAA).
No comments:
Post a Comment