LYON, Ufaransa
VURUGU jukwaani zilisababisha baadhi ya mashabiki kukimbilia sehemu ya
kuchezea na kuchelewesha kuanza kwa mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Ligi ya
Ulaya kati ya Lyon na Besiktas.
Hatahivyo, wenyeji ndio walikuja kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo
huo.
Vurugu zilitokea na kusababisha polisi kuingilia kati nje ya uwanja kabla
ya kuibukia nyuma ya goli ambako wachezaji walikuwa wakipasha.
"Vitu ukiwemo moto vilirushwa kutoka jukwaani nakusababisha baadhi
ya wapenzi kuwa wakimbizi kwa muda uwanjani ili kuokoa maisha yao, “ Lyon
walitweete.
Mchezo huo ulianza baada ya dakika 45 huku Lyon ikifunga mara mbili
katika dakika 10 za mwisho nan aibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mamlaka walitenaga maeneo yenye riski kubwa, ambapo askari 500 walimwagwa
kwenye Uwanja wa Parc Olympique Lyonnais ikiwa ni zaidi ya idadi ya kawaida.
No comments:
Post a Comment