Balozi wa DStv na Mshiriki pekee kutoka Tanzania aliyeshiriki mashindano
ya London Marathon yaliyofanyika jana jijini London Alphonce Simbu ameibuka mshindi wa tano
huku akivunja rikodi yake kwa kutumia muda wa 2:09.10 ambao ndio muda wake bora
zaidi tangu aanze kushiriki mashindano ya kimataifa.
Kabla ya hapo rekodi yake
ilikuwa muda wa 2:09.21 aliyoiweka mwaka jana kwenye mashindano ya Lake Biwa
Marathon nchini Japan.
Simbu ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu wa Mumbai Marathon
ameonesha umahiri mkubwa katika mashindano hayo hasa ikizingatiwa kuwa
mashindano hayo yalikuwa yanashirikisha vinara wengi wa riadha ulimwenguni
wakiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele Wakenya
Daniel Wanjiru, Bedan Karoki na Abel Kirui.
Mara baada ya ushindi huo salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika huku Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akisema kuwa
kampuni yake imeridhishwa sana na ufanisi aliouonesha katika mashindano hayo.
Alisema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo katika kumdhamini Simbu umezaa
matunda kwani kiwango cha mwanariadha huyo kimekuwa kikiimarika siku hadi siku.
“Tumefurahishwa sana na kiwango alichoonyesha Simbu kwenye London Marathon. Hii
ni ishara nzuri sana na tunaamini atafanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya
riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London Agosti mwaka huu.”
Kwa upande wake, meneja wa mwanariadha huyo Francis John alisema kuwa
ameridhishwa na kiwango alichoonesha Simbu na kwamba punde tu atakaporejea
wataanza maandalizi kwa ajili ya ushiriki wake katika mashindano ya Dunia
yatakayofanyika Agosti mwaka huu.
Katika mashindano hayo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Mkenya, Danie
Wanjiru (2:05:48) akifuatiwa kwa karibu na Kenenisa Bekele (2:05:57) na Bedan
Karoki.
Regards,
Shumbana.
No comments:
Post a Comment