KAMPUNI ya Multchoice-Tanzania kupitia kisimbuzi cha DStv wataonesha
mubashara mbio za Marathon za London, ambazo Mtanzania Alphonce Simbu
atashiriki.
Macho na masikio ya watanzania yataelekezwa jijini London, kumshuhudia
mwanariadha huyo akifanya vitu vyake katika mbio hizo kubwa.
Mbio hizi zitashirikisha wanariadha nyota duniani, ambao watawania kitita
cha zaidi ya sh Milioni 200 zitakazotolewa kwa mshindi wa kwanza.
Wanariadha nyota watakaoshiriki mbio hizo ni wale kutoka Kenya, Ethiopia
na Eritrea.
Mashindano hayo yataonekana Mubashara kupitia king’amuzi cha DStv katika chaneli namba 209 ya SuperSport (SS9)
kuanzia saa tano asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema kuwa
king’amuzi maarufu cha DStv kitaonesha mbio hizo ubashara `live’ nakuwawezesha
watu kuona moja kwa moja.
“Wakati wote DStv imekuwa kinara katika kuwahakikishia watanzania wengi
uhundo wa aina yake hususan katika ulingo wa michezo na burudani na kwa mara
nyingine tena tunauwezesha umma wa watanzania kushuhudia tukio hilo muhimu,
ambapo balozi wetu Simbu anatuwakilisha katika mashindano makubwa ya riadha,”
akisema Maharage.
Simbu ambaye pia ni Balozi maalum wa DStv, ni Mtanzania wa kwanza
kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered
Mumbai Marathon.
Katika mbio hizo za kesho, Simbu anatarajia kuwapa wakati mgumu
wanariadha nyota duniani watakaoshiriki mbio hizo.
Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo
la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki mashindano ya Dunia yatakyofanyika
jijini London Agosti.
Udhamini huo wa DStv ulianza tangu mwaka jana, ambapo mwanariadha huyo
amekuwa akipatiwa posho ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi yake ya mazoezi.
No comments:
Post a Comment