LONDON, England
KOCHA wa Newcastle Rafael Benitez (Pichani), anatakiwa kupewa fedha ili kuimarisha
kikosi chake kabla ya timu hiyo haijaanza msimu mpya katika Ligi Kuu, anasema
gwiji wa klabu hiyo, Alan Shearer.
Benitez alitumia zaidi ya kiasi cha pauni Milioni 50 katika kipindi
kilichopita cha majira ya joto baada ya timu hiyo kushushwa daraja, lakini
Shearer anasema kuwa kuna hatari ya kumkosa kocha huyo Mhispania, endapo
hatapewa fedha zaidi.
"Nafikiri kama atapewa fungu zaidi la usajili bila shaka kitakuwa
kishawishi kikubwa kwake kubaki katika timu hiyo, “alisema mchezaji huyo mwenye
rekodi ya kufunga mabao mengi katika timu hiyo.
Newcastle ilipanda daraja baada ya kushinda mabao 4-1 katika mchezo wa
nyumbani dhidi ya Preston uliofanyika Jumatatu.
Nahodha huyo wazamani wa England aliongeza: "Ni mtu mkubwa katika
klabu. Anapapenda mahali hapa na ni mvumilivu na muhimu zaidi ni kwa Newcastle
kuendelea kumbakisha.
"Nina uhakika atataka timu iimarishwe na atataka hilo lifanyike.”
"Watu wamebaini kuwa timu inahitaji kuimarishwa zaidi ili kufikia
pale wanapotaka kuwa, katika nusu ya juu ya Ligi Kuu.
"Sasa ni mahali ambako Newcastle inataka kuwa, kuwa katika Ligi Kuu
na hawataki kuwa katika nafasi tatu za chini, ambazo ni za kupambana dhidi ya
kushuka daraja.”
Winga wazamani wa Newcastle, Chris Waddle naye aliunga mkono maneno ya
Shearer, ambapo anaamini kuwa, Benitez atataka kuimarisha kikosi chake ili
kifanye vizuri.
Benitez aliteuliwa kuifundisha Newcastle Machi 2016 lakini alishindwa
kuiokoa timu hiyo kuteremka daraja hadi daraja la kwanza.
No comments:
Post a Comment