MADRID, Hispania
KOCHA wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amesema mwamuzi Viktor Kassai
hakuwajibika ipasavyo katika mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya na ametaka kuanza kutumika mara moja teknolojia ya video.
Kiungo wa Bayern Arturo Vidal alitolewa baada ya kuoneshwa kadi mbili,
wakati nyota wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo akifunga katika muda wa nyongeza akiwa katika eneo la kuotea wakati
mabingwa hao wa Ulaya wakisonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-3 jana.
Tulikuwa tukijia kila kitu wakati tukienda katika mchezo huu isipokuwa
mwamuzi tu, “alisema Ancelotti.
"Huwezi kuamua timu inayokwenda nusu fainali kwa mtindo kama huu.
Haiwezi kutokea katika kiwango hiki.”
Ancelotti, ambaye ni kocha wazamani wa Madrid, pia alisema kuwa kocha wa
Real Zinedine Zidane alikubaliana na tathmini yake kuhusu mwamuzi huyo wa
Hungary kushindwa kumudu mchezo huo kwenye Uwanja wa Bernabeu.
"Mwamuzi hakuwa kabisa katika mchezo na hakufanya kazi yake,
“alisema Ancelotti.
"Sifikiri kama Real Madrid ilikuwa na ushawishi wowote kwa waamuzi.
Waamuzi usiku huu wamechemsha, nilikuwa shishabikii matumizi ya teknolojia ya
video, lakini sasa nakiri kuwa inahitajika.”
Teknolojia ya goli inaamua kama mpira umevuka mstari, ambapo ilianza
kutumika katika Ligi kuu msimu wa mwaka 2013-14 na Bundesliga walianza kutumia
kuanzia mwaka 2015-16.
Na Uingerea pia wanatarajia kutumia videoa kwa ajili ya kumsaidia mwamuzi
kubadili maamuzi yake, ambapo hatua hiyo inatarajia kuanza katika kampeni za
mwaka 2017-18.
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge alimtuhumu Kassai kwa
“kuharibu mchezo.”
Alisema: "Ni jambo linalojia hasira kwa mwamuzi kushindwa kutoa
maamuzi ya haki….”
"Mchezo ulikuwa mzuri, lakini kwa bahati mbaya mwamuzi alitoa
maamuzi ambayo ni wazi ndio yaliyotugharimu. Mwamuzi ndiye aliyeharibu mchezo.”
Katika mchezo huo, Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu `hat-trick’
wakati mabingwa watetezi Real Madrid wakiipiku kitata Bayern Munich katika muda
wa nyongeza na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
`Hat-trick’ ya Ronaldo imemfanya mchesaji huyo kuwa wa kwanza kufikisha
mabao 100 katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Katika usiku huo, majirani wa Real Atletico nao walitinga nusu fainali ya
mashindano hayo baada ya kutoka sare ya 1-1 na Leceister City na kushinda kwa
jumla ya mabao 2-1 baada ya kushinda 1-0 mchezo wa kwanza.
No comments:
Post a Comment