BRUSSELS, Ubelgiji
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amekilaumu kikosi chake kwa
washambuliaji `kuchemka’ baada ya Anderlecht kufanikiwa kuifunga bao la
kusawazisha katika mchezo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Ulaya.
Man United ilikuwa mbele kwa bao 1-0 katika mchezo huo uliopigwa nchini
Ubelgiji hadi pale katika dakika ya 86 wakati wenyeji waliposawazisha baada ya
kulifikia lango hilo mara moja.
“Kama ningekuwa beki wa Manchester United ningeshangazwa sana na
washambuliaji, “alisema Mourinho.
Henrikh Mkhitaryan alipata nafasi nzuri ya kuifungia Manchester United
katika dakika ya 36, lakini hayo ndio yalikuwa mafanikio mazuri zaidi katika
mashuti 16 yatimu hiyo waliyopiga kwa mpinzani wake.
Wageni wako pointi nne nyuma ya wapinzani wao Man City waliopo katika
nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu ya England,ambapo wamefunga mabao 46.
Chelsea, Tottenham, Liverpool, Manchester City na Arsenal wote kila mmoja tayari imefunga mabao
zaidi ya 60.
Zlatan Ibrahimovic ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao katika
timu hiyo baada ya kufunga mabao 28 katika mashindano yote, lakini Mkhitaryan
na Juan Mata wanamfikia endapo ukilinganisha mabao yao yote.
"Ni matatizo hay ohayo, “aliongeza Mourinho. "Tulitawala
mchezo, na tulipata nafasi, lakini tlishindwa kufunga mabao ya kutosha.
"Katika lugha yangu dhaifu ya Kiingereza neno zuri la kusema sio
zaidi ya kuchemka. Tunatakiwa kuwa makini
No comments:
Post a Comment