Tuesday, 24 October 2017
Ronaldo, Zidane wang'ara tuzo za Fifa 2017
LONDON, England
CRISTIANO Ronaldo
ametangazwa kuwa ndiye mchezaji bora wa dunia wa kiume katika tuzo za
Shirikisho la Kimataifa la Soka 2017 zilizofanyika jijini hapa.
Mshambuliaji huyo
wa Real Madrid na Ureno aliwapiga kumbo mwenzake wa Barcelona Lionel Messi na
yule wa Paris St-Germain, Neymar katika mbio za kutwaa tuzo hiyo.
Ronaldo, 32,
aliisaidia Real Madrid kutwaa mataji mawili, likiwa lile le La Liga, ambalo
walilitetea na La Liga msimu wa mwaka 2016-17.
Lieke Martens wa
Barcelona na Uholanzi alishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wakike, huku
kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alitangazwa kuwa kocha bora wakiume na
Mholanzi Sarina Wiegman amekuwa kocha bora wakike.
Mchezaji wa
Arsenal Olivier Giroud alipokea tuzo ya Puskas kwa ajili ya bao lake bora 2017
walipocheza dhidi ya Crystal Palace Januari.
Tofauti ya Ballon
d'Or na Fifa?
Hii ni mara ya pili
kufanyika tuzo hizo za Fifa za soka, ambazo ni tofauti na zile za Ballon d'Or.
Tuzo ya Ballon
d'Or ilikuwa ikitolewa na jarida la Soka la Ufaransa tangu mwaka 1956, lakini
Fifa ilijitenga na tuzo hizo na kuanzisha zake.
Badala yake,
ilianzisha tuzo za tuzo za mchezaji bora wa Fifa, ambapo Ronaldo ndiye alikuwa
mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo Januari.
Kura za kumpata
mchezaji na kocha bora zinapigwa na manahodha wa timu za taifa na makocha,
waandishi wa habari walioteuliwa, na kwa mara ya kwanza, kura za katika mtandao
zilipigwa na mashabiki. Kila kundi lilikuwa na asilimia 25 ya kura.
Cristiano Ronaldo
Ni mwaka mwingine
wa kuvutia kwa Ronaldo, ambaye aliyetwaa tuzo ya kwanza ya mchezaji bora wa
Fifa wa Dunia baada ya kuiongoza Ureno kutwaa taji la Euro 2016.
Mwaka huu alifunga
mabao mawili wakati Real Madrid ikishinda 4-1 dhidi ya Juventus katika fainali
ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na pia alizifumania nyavu mara 25 katika mechi 29
alizoichezea klabu yake katika La Liga ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika miaka
mitano.
"Tuko England
kwa mara ya kwanza, na tumeshinda kwa mara ya pili mfululizo. Huu ni wakati
mzuri kwangu, “alisema Ronaldo alipokuwa akizungumza wakati wa kukabidhiwa tuzo
hiyo.
Wachezaji watatu
wakiume
Cristiano Ronaldo
- 43.16 % Lionel Messi - 19.25 % Neymar - 6.97%
Messi alimpigia
kura mchezaji mwenzake wa Barcelona Luis Suarez kama mchezaji bora, wakati
Ronaldo naye pia alimpigia mchezaji mwenzake wa Real, Luka Modric.
Kocha wa England
Gareth Southgate alimpigia kura Ronaldo.
Mchezaji bora
wakike
Martens, 24,
alikuwa mhimili wa timu ya taifa ya Uholanzi katika ushindi wa timu hiyo katika
mashindano ya Mataifa ya Ulaya, ambapo alishinda tuzo ya mashindano hayo.
Fifpro World XI
Fifa imefanya
mabadiliko matatu katika kikosi cha mwaka 2016. Kipa Gianluigi Buffon
alimbadili Manuel Neuer, wakati mchezaji wa AC Milan Leonardo Bonucci
alimbadili mchezaji wa Barcelona, Gerard Pique katika nafasi ya beki bora na
mchezaji wa PSG Neymar ameshika nafasi ya ushambuliaji bora hiyo badala ya Luis
Suarez.
Orodha ya
wachezaji hao watano ni kutoka Real Madrid, wawili Barcelona, wawili PSG, mmoja
Juventus na mmoja AC Milan. Hakuna mchezaji wa Ligi Kuu ya England aliyomo
katika kikosi hicho.
Kocha bora
Real ilimaliza
msimu uliopita ikiwa bingwa wa Hispanuia na kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012
na kutwaa ubigwa wa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo.
Zidane alishinda
tuzo hiyo akimshinda kcha wa Chelsea Antonio Conte, ambaye alitwaa taji la Ligi
Kuu katika msimu wake wa kwanza England, na yule wa Juventus, Massimiliano
Allegri, aliyeiongoza timu yake kutwaa mataji mawili ya Serie A na lile la
Coppa Italia.
Zinedine Zidane -
46.22% Antonio Conte - 11.62% Massimiliano Allegri - 8.78%
Kocha bora wakike
Mholanzi Wiegman
alioongoza timu yao ya taifa kutwaa taji la Euro 2017 katika ardhi ya nyumbani,
ambapo timu hiyo ilicheza soka safi la kuvutia.
Hilo lilikuwa taji
lao la kwanza kubwa la kimataifa kwa timu ya wanawake baada yakuifunga Denmark
katika fainali.
Tuzo ya Puskas
Bao bora la mwaka
2017 ni lile lililofungwa na mchezaji wa Arsenal, Giroud.
Bao hilo
lilifungwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Palace siku ya mwaka
mpya, ambapo mshambuliaji huyo Mfaransa alifunga bao safi aliunganisha krosi ya
Alexis Sanchez niliyopigwa nyuma yake.
Kipa bora
Bingwa wa Kombela
Dunia, na mshindi mara 10 wa taji la Serie A, Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa
kwanza wa tuzo ya kipa bora.
Kipa huyo mkongwe
aliisaidia Juventus kutwaa mara sita mfululizo taji la Serie A na kucheza
dakika 600 bila kuruhus bao katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Buffon, 39, alitwaa
tuzo hiyo akiwashinda Keylor Navas, Manuel Neuer, aliyeisaidia Bayern Munich
kutwaa Bundesliga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment