Sunday, 1 October 2017
Chaneta waibuka na mikakati ya kuinua netiboli
UONGOZI mpya wa
Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) umesema kuwa umejipanga kuhakikisha
unaleta maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.
Akizungumza jana Katibu Mkuu mpya wa Chaneta, Judith Ilunda (pichani) alisema kuwa,
wanajua changamoto zilizopo katika chama hicho, lakini wamejipanga kukabiliana nazo ili kuleta maendeleo katika mchezo huo.
Ilunda ambaye ni
mchezaji wazamani wa timu ya Bandari Dar na timu ya taifa ya netiboli kwa muda
mrefu, alisema kuwa watahakikisha mchezo huo unachezwa katika shule za msingi,
sekondari na mitaani.
Alisema pia
watahakikisha wanaendesha mashindano ya mara kwa mara na timu zenye ubora
zinashiriki, ili kuhakikisha mchezo huo unarudi katika chati kama zamani
kitaifa na kimataifa.
Alisema kamati yao
mpya itakutana hivi karibuni mara baada ya kukabidhiwa ofisi na uongozi
uliopita na kutangaza zaidi mipango yao ya muda mrefu na mfupi.
Uchaguzi Mkuu wa
Chaneta ulifanyika mjini Dodoma juzi, ambapo Dk Devetha Marwa aliutwaa uenyekiti baada ya kupata kura 53
dhidi ya Damian Chonya aliyepata kura nne.
Makamu ni Anna
Gidaria aliyepata kuta 44 dhidi ya Winfrida Emmanue kura 10 na Pili Mogella
alipata kura tatu.
Nafasi ya Katibu
Mkuu ilikwenda kwa Ilunda aliyepata kura 50 dhidi ya makamu mwenyekiti
aliyepita Zainabu Mbiri aliyeambulia kura sita, huku katibu msaidizi ni Hilda
Mwakatobe aliyepata kura 30 dhidi ya 26 za Mwajuma Kisengo.
Nafasi ya mhazini
haijajazwa baada ya mgombea pekee, Grace Khatibu kupata kura nne za ndio na
hapana 49 na hivyo kutoweza kuchaguliwa kwa kuwa alikuwana kura nyingi za
hapana.
Wapiga kura walikuwa 57 kutoka mikoa 21 ya Tanzania Bara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment