Monday, 2 October 2017
50 wauawa Marekani kwa risasi wakicheza muziki
ANGALAU watu 50 wameuawa
na wengine 200 kuumia vibaya katika shambulio la watu wengi lililotokea jijini
hapa katika onesho la wazi la muziki.
MTU mwenye silaha, aliyejulikana kwa jina la Stephen Paddock mwenye
umri wa miaka 64, alimimina risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay Hotel
kuelekea katika tamasha la wazi la muziki.
Polisi imesema kuwa mtu huyoaliyetambulika kama mkazi wa eneo hilo,
naye aliuawa kwa risasi na maofisa polisi.
Sheriff Joe Lombardo alisema kuwa hawezi kujua idadi kamili ya watu waliokufa au kuumia,
lakini alithibitisha maofisa wawili ni miongoni mwa waliokufa.
Msemaji wa hospitali ya hapa
alisema mpema kuwa angalau watu 14 kati ya walioumia walikuwa katika hali mbaya
sana.
Kulikuwa na ripoti za matukio hayo
katika maeneo tofauti tofauti pamoja na Las Vegas, lakini polisi ilisema kuwa taarifa hizo zilikuwa za uongo.
Shuhuda, Mike Thompson kutoka London, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, kuwa aliona watu wakikimbia
wakiwa wamechanganyikiwa.
"Mtu mmoja
alikuwa amejawa damu mwili mzima na nilijua kuwa kuna tatizo kubwa.
"Watu walikimbia
na kuwa na vurugu.”
Baadhi ya ndege zilibadili safari baada
ya kusambaa kwa taarifa za tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment