Tuesday, 10 October 2017
Messi apiga hat-tric Argentina ikifuzu Kombe la Dunia
QUITO, Ecuador
QUITO, Ecuador
LIONEL Messi
amefunga hat-trick wakati Argentina ikitoka nyuma na kushinda ugenini 3-1 dhidi
ya Ecuador na kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia
mwakani.
Brazil wenyewe
tayari walishafuzu huku Luis Suarez akizifumania nyavu mara mbili wakati Uruguay
ikiichapa Bolivia 4-2 na kufuzu, pamoja na Colombia nayo pia ikifuzu licha ya
kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Peru.
Peru ilimaliza
mchakato huo ikiwa katika nafasi ya tano ya Kanda ya Amerika Kusini ya kufuzu
kwa Kombe la Dunia na sasa itakutana na New Zealand katika mechi mbili za
mchujo zitakazochzwa nyumbani na ugenini.
Lakini Alexis
Sanchez na Chile wametupwa nje baad aya kupokea kichapo cha mabao 3-0 ugenini
dhidi ya Brazil.
Argentina ilianza
siku ikiwa katika nafasi ya sita na kuwa katika hatari ya kuweza kushindwa
kufuzu kwa Kombela Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1970.
Timu hiyo ilianza
vibaya katika mchezo huo uliofanyika katika ukanda wa juu uliopo hapa na
wenyeji walikuwa mbele katika sekunde ya 38 kupitia kwa Romario Ibarra likiwa n
bao la mapema zaidi kufungwa Argentina katika Kombe la Dunia.
Hatahivyo, Argentina,
ambao ni washindi wa pili wa Kombe la Dunia mashindano yalipofanyikia nchini
Brazil 2014, walipambana huku Messi akiwa katika kiwango cha hali ya juu.
Messi, ambaye ni
bingwa mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia, alisawazisha baada
ya dakika 12 baada ya kushirikiana vizuri na kiungo wazamani wa Manchester
United Angel di Maria.
Bao lake la pili
lilikuja dakika nane baadae kwa shuti kali ndani ya eneo la hatari kabla
hajafunga la tatu na kuiwezesha timu yake kufuzu kwa fainali za mwakani za
Kombe la Dunia.
MAJAGA
KWA CHILE
Chile,ambayo
ilitwaa taji la Copa America katika mashindano mawili yaliyopita, ilikuwa
nalengo la kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo katika Kombe la Dunia baada ya mara
ya mwisho kucheza hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014.
Walianza raundi
hiyo ya mwishi wakiwa katika nafasi ya tatu, lakini walishindwa baada
yakufungwa mabao mawili na Brazil ndani ya sekunde tatu yaliyofungwa na Paulinho
na Gabriel Jesus.
Wakati Peru
ikifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho za mchezo huo dhidi ya
Colombia, Chili ilikuwa ikihitaji kufunga tu ili kucheza hatua ya mtoano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment