Monday, 23 October 2017
Mkurugenzi TAA ataka Tughe kutetea wafanyakazi
Na Mwandishi Wetu
KAIMU Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela
amewataka viongozi wa Chama cha Wafanyakazi kusikiliza malalamiko
ya wafanyakazi
bila kubagua.
Bw.Mayongela
alisema viongozi wa Wafanyakazi kupitia matawi mawili ya Chama cha Wafanyakazi,
TAA Makao Makuu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
kutenda haki kwa kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi wote na kuyawasilisha kwa
wasilisha kwa mwajiri ili yafanyiwe kazi.
Alitoa kauli hiyo
juzi wakati viongozi wa matawi hayo walipokwenda kujitambulisha ofisi kwake TAA
Makao Makuu, ambapo alisisitiza kuwa wafanyakazi wa chini ndio wenye matatizo
makubwa, lakini hawasikilizwi na kutatuliwa matatizo yao kwa wakati.
“Ninashukuru
uongozi mmekuja kuonana nami, ninahitaji ushirikiano wenu kama Chama cha
Wafanyakazi, muwatumikie wafanyakazi kwa kutenda haki mkisikiliza matatizo ya
kila mmoja na kufikisha sehemu husika na ninawaahidi kuwa nanyi bega kwa bega
kutatua matatizo ya wafanyakazi kwani wao ndio wanafanya TAA iwepo, “alisema
Mayongela.
Alisema
wafanyakazi endapo wakifanya kazi bila manung’uniko wala makundi, mamlaka
itasonga mbele kwa kuwa na uongozi sio kupigana vita bali unatakiwa kujijenga
na kuwa kitu kimoja.
Hatahivyo alisema
kwa sasa yupo mbioni kuangalia namna ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupitia makusanyo yatakayotokana na
vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuongeza tija na ufanisi wa kazi ili kuongeza
ari kwa wafanyakazi.
Aliendelea kusema
kuwa inaonekana wafanyakazi wengi wa TAA wamekata tamaa kutokana na kufanya kazi
nyingi na wakati mwingine kupitiliza muda wa kazi wa kawaida bila kupata
stahiki yeyote.
“Kwa msaada wa
Mungu nina imani atanionyesha wapi fedha zilipo na jinsi ya kuzitumia ipasavyo
kwa masuala ya msingi, na ninakusudia hadi kufika Desemba mwaka huu niweze
kuboresha maslahi ya wafanyakazi.
Watu wanafanya
kazi sana lakini maslahi ni madogo, unaona kabisa jinsi mtu anavyoitumikia
taasisi kwa moyo, lakini sura inaonesha jinsi alivyokata tamaa, ninaamini kwa
kufanya hivi itaongeza tija na bidii ya kazi.” Alisema Bw. Mayongela.
Halikadhalika, Bw.
Mayongela amesema atahakikisha wafanyakazi wanapata vitendea kazi vya uhakika
kulingana na kazi zao, zikiwemo bajaji, pikipiki na magari kwa ajili ya doria
na shughuli za uendeshaji ndani ya Viwanja vya Ndege.
Pia amewataka
viongozi hao kuwa karibu na wafanyakazi ili kuhakikisha wanawahamasisha
wanafanya kazi kwa bidii, uaminifu na uadilifu ili kuondoa mianya na tabia za
upokeaji wa rushwa, kwa kuwa TUGHE ni daraja kati ya mwajiri na wafanyakazi.
Naye Mwenyekiti wa
TUGHE tawi la TAA Makao Makuu, Bw. Nasib Elias mbali na kumshukuru Kaimu
Mkurugenzi Mkuu kwa kuwapa fursa ya kukutana naye, lakini alimuomba kuendelea
kudumisha mahusiano baina ya mwajiri na Tughe.
Pia alimuomba
aitake menejimenti yake kuwa na utaratibu wa kuweka milango wazi kwa
wafanyakazi kama yeye ili waweze kusikiliza na kutoa majibu sahihi kwa baadhi
ya masuala ya kiofisi yanayowasilishwa na wafanyakazi kwao na sio kila jambo
liwasilishwe kwake.
“Tunakuombea kwa
Mungu akutie nguvu kwa haya unayotaka kufanya likiwemo la kuboresha maslahi ya
wafanyakazi kwa kuwa litasaidia kuamsha morali ya kazi kwa wafanyakazi, lakini
hii sera yako ya kuwacha milango wazi, tunaomba nayo itekelezwe katika ngazi ya
menejimenti yako kwani kuna mambo ambayo yanaweza kumalizwa na Wakurugenzi na
Mameneja wenyewe na sio lazima yafike kwako, “ alisema Bw. Elias.
Katika kuboresha
maslahi ya wafanyakazi ambacho kimeonekana ni kipaumbele cha Kaimu Mkurugenzi
mkuu kwa wafanyakazi, Bw. Elias amemuomba kuangalia namna bora ya kusimamia
maslahi hayo ikiwemo kuuasili mkataba wa hali bora (SBA) kama inavyotekelezwa
na taasisi nyingine za serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment