Neymar akioneshwa kadi nyekundu wakati PSG ilipocheza dhidi ya Olympique de Marseille. |
Monday, 23 October 2017
Neymar atolewa wakati PSG ikitoka sare
NEYMAR alitolewa
nje kabla ya mchezaji mwenzake Edinson Cavani akithibitisha thamani yake kwa
mara nyigine tena kwa kufunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho wakati
Paris St Germain (PSG) ikitoka sare ya 2-2 dhidi ya wapinzani wao wakubwa
Olympique de Marseille.
Mshambuliaji huyo
wa Uruguay alisawazisha dakika moja ndani ya muda wa nyongeza kwa shuti kali la
umbali wa kama meta 20 baada ya Neymar kutolewa nje katika dakika ya 87 kwa
kadi ya pili ya njano.
Neymar ndiye
alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 33
kufuatia lile la kuongoza la Olympique de Marseille lililofungwa na Luiz
Gustavo katika dakika ya 16.
Awali, Marseille
walifunga bao la pili katika dakika ya 78 lililowekwa kimiani na Thauvin,
ambalo baadae PSG walisawazisha kupitia kwa Cavan na kunusurika kupata kipigo
cha kwanza.
Kimsimamo, PSG ina
pointi 26 baada ya kucheza mechi 10 ikiwa kileleni pointi nne zaidi ya Monaco
iliyopo katika nafasi ya pili.
"Ni bao
muhimu kwani mchezo ni kama ulikuwa umemalizika, lakini angalau tumeondoka na
pointi, “alisema Cavani.
Monaco wako nafasi
ya pili, pointi nne nyuma wakiwa na pointi 22 baadaya kuifunga Caen 2-0
Jumamosi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment