Friday, 27 October 2017
Fifa yaongeza zawadi Kombe la Dunia
ZURICH, Uswisi
MATAIFA 32 yatakayoshindana
katika fainali za Kombe la Dunia 2018 yatagawana kiasi cha dola za Marekani
milioni 400 (sawa na sh bilioni 898) katika zawadi ikiwa ni ongezeko la asiliia
12 ya fedha za mashindano ya mwaka 2014, Fifa imesema.
Katika taarifa
yake jana Shirikisho hilo la Kimataifa la Soka limesema kuwa fedha zawadi
katika mashindano yaliyopita yaliyofanyika Brazil zilikuwa dola za Marekani
milioni 358.
Imeelezwa kuwa
Ujerumani ambaye ni bingwa wa Kombe la Dunia alindoka na kitita cha dola za
Marekani milioni 35, huku mshindi wa pili Argentina alipata dola milioni 25.
Tofauti, nchi
ambazo zitashindwa kuvuka hatua ya makundi kila moja itapokea kiasi cha dola za
Marekani milioni 8.
Katika mkutano wa
Fifa uliofanyika Kolkata, bodi hiyo ya Fifa pia imepitisha taratribu za kuomba
uenyeji wa Kombe la Dunia kwa ajili ya mwaka 2026.
Huku ikithibitisha
tarehe za mashindano mbalimbali, yakiwemo ya Kombe la Dunia yatakayofanyika
Falme za Kiarabu na yale ya wanawake ya mwaka 2019 yatakayofanyika Ufaransa.
Fainali za Kombela
Dunia za mwaka 2018 zitafanyika kuanzia Desemba 12 hadi 22, wakati yale ya
wanawake ya mwaka 2019 yamepangwa kufanyika kuanzia Juni 7 huku fainali
ikifanyika Julai 7.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment