Monday, 16 October 2017
Waegesha ndege 10 wa JNIA wapigwa msasa
Na Mwandishi Wetu
WAEGESHA ndege 10
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo walianza
mafunzo ya siku saba ya uegeshaji ndege kutoka kwa wakufunzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Hague cha Uholanzi yanayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga
(CATS) jijini Dar es Salaam.
Akifungua mafunzo
hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amesema kuwa mafunzo
hayo ni muhimu kwani yatazidi kuwajengea uwezo na uzoefu washiriki hao.
Bw. Mayongela
amewasisitiza washiriki hao kuzingatia kila wanachofundishwa ili waweze kuwa
mahiri na weledi katika uongozaji wa ndege za ndani na nje ya nchi zinazotumia
kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
“Waongoza ndege ni
moja ya kazi inayohusisha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya watoa huduma
ndani ya kiwanja cha ndege, hivyo ni lazima tufikie viwango vinavyotakiwa kwa
mujibu wa sheria kimataifa,” amesema Bw. Mayongela.
Hata hivyo,
amesema TAA inajukumu kubwa la kuwaongezea uwezo watumishi wake kwa kuwapeleka
kwenye mafunzo mbalimbali ili kujijengea uwezo na maarifa.
Bw. Mayongela
amewashukuru waendeshaji wa mafunzo hayo yanayotolewa na mfuko wa Avi Assist wa
Uholanzi, ambapo amewahahakikishia kuendeleza ushirikiano waliouanzisha kwa
kushirikiana katika utoaji wa mafunzo ya kada mbalimbali.
Naye Mkuu wa
Kitengo cha Waongoza ndege cha JNIA, Bw. Lugano Mwinuka amesema mafunzo haya
yamekuja wakati muafaka, kwa kuwa walikuwa yakiyahitaji kwa muda mrefu, na sasa
anauhakika wa washiriki wataongeza ujuzi katika utendaji wao wa kazi.
Bw. Mwinuka
amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa nadharia na vitendo, ambapo washiriki hao
wamegawanywa katika makundi mawili ya watu watano, ambao ni Earisner Waihula,
Emmanuel Nyaulingo, Anunciatus Alex, Fadhili Meena na Oscar Kibiki.
Watakaoingia kundi
la pili ni pamoja na Denis Kinyaga, Zennobius Mwimba, Raynard Komba, Said Mussa
na Meshack Elisante.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment