Sunday 26 July 2015

Mtoto wa Whitney Houston afariki dunia

*Kifo chake kimetokea baada ya kuchomolewa mashine


NEW YORK, Marekani
MTOTO wa mwanamuziki Whitney Houston (sasa marehemu), Bobbi Kristina Brown amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 22, alisema mwakilishi wa familia.

Msemaji wa familia hiyo Kristen Foster alisema Kristina alifariki dunia akiwa amezungukwa na familia yake na "hatimaye ana amani katika mikono ya Mungu ".

Brown alikutwa akiwa ajitambui katika bafu Januari 31 na tangu wakati huo alikuwa katika koma. Kamwe hakuwahi kuzinduka tangu wakati huo.
 
Baadae alihamishiwa katika hospitali ya wagonjwa mahututi katika jiji la Duluth, Georgia, mwezi mmoja uliopita baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.

Brown ni mtoto pekee wa kike wa Houston aliyezaa na muimbaji nyota wa R&B Bobby Brown.

Whitney Houston alikutwa amekufa katika bafu la hoteli huko Los Angeles mwaka 2012.

"Bobbi Kristina Brown alifariki Julai 26 2015, akiwa amezungukwa na familia yake, " alisema Foster.

"Hatimae amepumzika kwa amani katika mikono y Mungu. Tunapenda kumshukuru kila mmoja kwa upendo wake na kutuunga mkono katika kpindi hiki cha miezi kadhaa ya matatizo."

Taarifa zingine kutoka Los Angeles zinasema Brown alikuwa na ndoto za kufuata nyayo za mama yake katika uimbaji na uigizaji, na tayari alikuwa na majukumu kidogo katika TV, lakini bado alikuwa hajaanza kuchanganya.

Lakini Januari Polisi walisema kuwa Brown alikuwa uso wake ukiwa chini bafuni nyumbani kwake Atlanta ambako alikuwa akishirikiana na Nick Gordon, mtu ambaye alikuwa akimuita mume wake.

Gordon alisema wakati huo kuwa alionekana kutopumua kabla ya kuwasili kwa huduma ya dhahrura.

Brown aliwekwa eneo la wagonjwa mahututi akipatiwa matubabu ambako alikuwa akipumua kwa kutumia mashine.

Inaelezwa kuwa kifo chake kimetokea karibu miezi sita baada ya polisi na watu wa uokoaji kupigiwa simu Januari 31, 2015 kwenda kumchukua baada ya kukutwa amepoteza fahamu ndani ya bafu.
 
Tangu wakati huo mtoto huyo wa muimbaji nyota alikuwa akiishi kwa msaada wa mashine na inaelezwa kuwa alikuwa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya.
 

No comments:

Post a Comment