Sunday, 19 July 2015

Bartomeu ndiye rais wa Barcelona baada ya kumbwaga Joan Laporta


BARCELONA,Hispania
JOSEP Maria Bartomeu (pichani), amechaguliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa, rais wa klabu ya Barcelona, akimbwaga rais wazamani Joan Laporta katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki.
 
Barcelona ilisema katika katika moja ya chaneli zake za telivisheni kuwa, Bartomeu alipata wastani wa asilimia 54.63% ya kura zilizopigwa na wanachama wa klabu hiyo.

Bartomeu mwenye umri wa miaka 52 ambaye sasa ataongoza klabu hiyo kwa miaka sita ijayo.

Rais huyo wa Barcelona alichukua uongozi huo Januari mwaka 2014 kutoka kwa Sandro Rosell, aliyeachia ngazi kufuatia kashfa ya usajili wa Neymar.

Laporta ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Bartomeu katika uchaguzi huo, alipata asilimia 33.03 ya kura zilizopigwa.

Bartomeu, aliyejiuzulu mwezi uliopita wakati bodi ya muda ikiongoza klabu hiyo wakati wa kipindi cha uchaguzi, atarejea ofisini na kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni za kuwania kiti hicho.

Barcelona ilithibitisha kuwa jumla ya kura 47,270 zilipigwa wakati wa uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment