LONDON, England
HATIMAYE mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester
United Robin van Persie kwenda Fenerbahce umekamilika, kwa mujibu wa taarifa za
vyombo vya habari vya Uturuki.
Mwenyekiti wa Fenerbahce Aziz Yildirim alisema
kuwa makubaliano yalikamilika tangu Ijumaa na mchezaji huyo wa kimataifa wa
Uholanzi, leo Jumapili anatarajia kutua Istambul kwa ndege binafsi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili wake.
"Tulifanya kazi kwa nguvu, hadi usiku wa
manane. Hatima ye tumefanikiwa kumsajili mcheaji huyo," alisema Yildirim
alipokaririwa na gazeti moja.
"Uhamisho wa van Persie umefanyika na
nyota mmoja zaidi ametua katika timu ya Fenerbahce.”
Van Persie Alhamisi alifanyiwa vipimo vya
awali vya afya England na alitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne wa
kuitumikia klabu hiyo ya Uturiki, lakini uhamisho rasmi ulikuwa nado haujathibitishwa.
No comments:
Post a Comment