BARCELONA, Hispania
LIONEL Messi yuko vizuri zaidi mwaka huu kuliko alivyokuwa mwaka 2009,
kwa mujibu wa winga wazamani wa Barcelona, Lobo Carrasco.
Mchezaji huyo aliiwezesha timu hiyo msimu uliopita kutwaa mataji matatu
kama alivyofanya miaka sita iliyopita wakati wa msimu wa kwanza wa kocha Pep
Guardiola, lakini Carrasco anaamini kuwa mshambuliaji huyo sasa amekamilika zaidi.
"Leo Messi wa sasa amekamilika zaidi, " alisema.
"Anaweza kukumaliza hata akiwa umbali wa mita 40 kutoka katika
goli, na sio kwa sababu amechukua mpira na kuanza kuukokota kuwapita wapinzani,
lakini kwa sababu anaweza kutengeneza nafasi ya kufunga goli.
Messi awali alikuwa akipambana kusaka kiwango katika nusu ya kwanza
ya msimu uliopita lakini alibadilika nusu ya pili ya msimu na kufanya vizuri.
"Barcelona walitarajia mambo mazuri msimu uliopita lakini sio
kutwaa mataji matatu. Ilikuwa inanekana kama haiwezekani kufikia mafanikio ya msimu
wa ajabu wa mwaka 2009, lakini Messi ndio aliuwa mhimili wa mafanikio."
Carrasco alitwaa mataji 10 wakati alipoichezea Barcelona mechi zaidi
ya 300, ikiwemo taji la La Liga mwaka 1985.
Pia alifikia fainali za Ulaya mwaka 1984, ambako Hispania ilifungwa
na wenyeji Ufaransa kwa bao la Michel Platini.
No comments:
Post a Comment