Mratibu wa dini wa ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania, Muhammed Cicek (wa pili kushoto) wakati ugawaji wa futari kwa wakati za Ilala jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wanawake wa Kiislamu wa Ilala wakisubiri kukabidhiwa futari zao zilizotolewa na ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania. |
Mwenyekiti wa taasisi ya Forum For Balance and Sustainable Development, Imamu Faraji Tamimu (kushoto) akizungumza jambo wakati wa utoaji wa futari hizo. |
Na Seba Nyanga
WAISLAMU wa Uturuki kupitia ubalozi wao
nchini Tanzania wametoa futari yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 30 katika
mkoa wa Dar es Salaam, imeelezwa.
Kwa mujibu wa mratibu wa dini wa ubalozi wa
Uturuki nchini, Muhammed Cicek, futari hiyoitawanufaisha waumini wa Kiislamu
1800 wa wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Alisema kila wilaya waumini 600 wamefaidika
na zoezi hilo ambalo kwa upande wa Ilala lilifanyika katika msikiti wa Masjid
Taqwa, ambapo mwakilishihuyo aligawa maboksi ya futari kwa waumini hao.
Akizungumza kabla ya kugawa futari hiyo
mwakilishi huyo aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuwa na mshikamano
miongoni mwao na kuwasaidia wasiojiweza kipindi hiki cha mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
Akigawa chakula hicho kwa niaba ya taasisi ya
Hasene ya Uturuki, Cicek alisema kwamba
wametoa msaada huo sio kwa sababu ya uwezo mkubwa wa kifedha waliokuwa nao ama
umasikini wa Watanzania, bali kuendeleza mshikamano miongoni mwa waumini wa Kiislamu
Tanzania.
Cicek aliwataka waislamu wa Tanzania
kuwaombea waislamu wengine wanaopoteza maisha kwenye nchi za Palestina, Syria,
Iraq na kwingineko.
Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Forum For
Balance and Sustainable Development, Imamu Faraji Tamimu alitoa rai kwa
waislamu nchini kote kuendelea kuwaombea wenzao wa Uturuki kupitia taasisi yao
ya Haseni kwa msaada wa chakula walioutoa wakati huu wa Ramadhani.
“Wenzetu wa Uturuki wametupa msaada huu sio kwa
sababu ni matajiri ila kwa sababu ya moyo wa upendo kwa Waislamu wenzao, “alisema Imamu Tamimu.
No comments:
Post a Comment