Tuesday 14 July 2015

Raheem Sterling kuvaa jezi namba 7 Manchester City



Mchezaji Raheem Sterling akionesha jezi namba saba atakayovaa Manchester City baada ya kukamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa kuanza kuitumikia timu hiyo, ambayo itamlipa mshahara wa pauni 180,000 kwa wiki.
LONDON, England
RAHEEM Sterling amekamilisha uhamisho wake kwenda Manchester City wa kitita cha pauni milioni 49 huku yeye akiondoka na pauni 180,000 kwa wiki kama mshahara wake.

Mchezaji huyo ambaye alipokuwa Liverpool alikuwa akilipwa chini ya pauni 80,000 na baadae kuahidiwa kuongezwa hadi 100,000 kama angeendelea kuitumikia timu hiyo, aligoma kubaki Anfield.
Raheem Sterlin akiwa na timu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ya Man City.
Mwakilishi wa Sterling, Aidy Ward alizungumza hadharani kuwa mchezaji huyo hakuwa na furaha hapo Anfield wakati wakielekea mwishoni mwa msimu uliopita, ambapo alisema kuwa mcheaji wake hata akiongezwa pauni 900,000 kwa wiki, hatabaki Liverpool.

Ward pia alidai kuwa kiungo huyo hakuwa na uhusiano mzuri na kocha wake Brendan Rodgers, lakini madai hayo yalikanushwa na kocha huyo wa Liverpool.
 
Lakini kufuatia vipimo vya afya katika klabu ya Man City, Sterling aliuambia mtandao wa klabu hiyo: ‘Napenda kuwashukuru watu wote wanaonizunguka, mama yangu na dada zangu, uongozi wa timu, na Aidy Ward kwa kunisaidia na kufika nilipo leo. 

Nimefurahi kwa mambo yote kukamilika.

Sterling mwenye umri wa miaka 20, aliweka wazi nusu ya pili ya msimu kuwa, hana mpango wa kuongeza mkataba Liverpool na katika mahojiano katika televisheni Aprili mwaka huu kuwa kinachomuondoa Liverpool sio pesa.

Laklini, baada ya kukamilisha kuondoka Liverpool, Sterling ametumia muda wake kumpongeza Rodgers.

‘Napenda kumshukuru Rafa Benitez kwa kunipeleka Liverpool wakati nikiwa na umri wa miaka 15 na Kenny Dalglish for kwa kuonesha imani kwangu wakati nikiwa na umri mdogo.
 
Mwisho napenda kumshukuru Brendan Rodgers kwa kunipatia nafasi ya kudumu katika timu ya kwanza na kukionesha duniani kipaji changu.

Sterling, atakayevalia jezi namba 7 katika timu hiyo yenye maskani yake kwenye uwanja wa Etihad na kufuzu vipimo vya afya kabla yakusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuondoka na pauni 180,000 kwa wiki, alisema anaangalia mbele kukutana na wachezaji wenzake wapya.

Mchezaji huyo alikiri kuwa alizungumza na kipa Joe Hart kuhusu kuhamia katika klabu hiyo wakati walipokutana katika timu ya taifa ya England.

No comments:

Post a Comment