Tuesday, 19 September 2017
Tetemeko la Ardhi laua Watu 140 nchini Mexico
MEXICO CITY,
Mexico
TETEMEKO kubwa la
ardhi limeikumba Mexico na kupoteza maisha ya zaidi ya watu 140 na kuharibu
majengo mengi katika jiji hili, imeelezwa.
Angalau watoto 21 wanahofiwa
kufa na wengine wakiripotiwa kupotea baada ya shule kuanguka katika jiji hilo.
Tetemeko hilo
linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa magnitude 7.1 pia limesababisha uharibifu
mkubwa katika nchi za jirani.
Kwa mara ya mwisho
tetemeko kubwa kama hilo liliwahi kutokea takribani miaka 32 iliyopita baada ya
tetemeko kuua maelfu ya watu Mexico City.
Hilo ni tetemeko
la pili kutokea baada ya lile la mapema mwezi huu ambalo lilikuwa na ukubwa na
magnitude 8.1 ambalo liliua watu 90 lilitokea kusini mwa nchi hii.
Angalau watu 149
wamekufa nchi nzima, kimeeleza chanzo kimoja cha habari.
Angalau watu 55
wamekufa katika Jimbo la Morelose,kusini mwa Mexico City, huku 32 wakifa huko Pueblae.
Watu 49 wanahofiwa kupoteza maisha Mexico City, huku wengine 10 wakifa katika
Jimbo la Mexico, na watau wakifa huko Guerrero.
Karibu watu
milioni 2 wakazi wa Mexico City wameachwa bila ya umeme huku nyaya za simu
zikiwa zimeanguka. Wananchi wameonywa kutovuta sigara mitaani kwani gesi
inaweza kulipuka.
Meya wa Mexico
City Miguel Angel Mancera aliaimbia TV moja kuwa huduma za uokoaji zinaendelea
kuchimba katika makazi 44 ili kuona kama kuna watu wamefukiwa na kifusi.
Kaimu Katibu wa
Elimu Javier Treviño, alikaririwa na vyombo vya habari vya haba kuwa, watoto 21
na watu wazima wanne walikufa wakati shule ya Enrique Rebsamen iliyopo kusini
mwa Mexico City ilipoanguka.
Baadhi ya
wanafunzi waliokolewa, vyombo vya habari vya Mexico viliripoti, lakini wengine
bado hawajapatikana.
Nyumba za gholofa,
maduka makubwa na kiwanda navyo pia ni baadhi ya vitu vilivyoanguka jijini
hapa.
Akihutubia kupia
televisheni, Rais wa Mexico Peña Nieto alisema dharura imechukulia katika
maeneo yaliyoathirika na jeshi limekwenda kutoa msaada.
Karibu sehemu zote
katika jiji la Mexico, timu ya watu wa uokoaji na wake wakujitolea wamekuwa
wakifanya jitihada mbalimbali kuwaokoa watu.
"Mke wangu
yuko pale. Sijaweza kuwasiliana naye, “alisema Juan Jesus Garcia, 33, huku
akitokwa na machozi jirani na jengo lililoanguka.
"Hajaweza
kujibu simu na sasa tumeambia kuzima simu zetu za viganjani kwa sababu kuna
gesi inayovuja inaweza kulipuka.”
Tetemeko hilo la ardhi
limetokea jijini Mexico wakati wa
kumbukumbu ya miaka 32 ya tetemeko jingine la ardhi lililoua watu 10,000.
Mexico City ni
moja ya majiji yenye watu wengi duniani, ambapo ina zaidi ya wakazi milioni 20
wanaoshi hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment