Na Mwandishi Wetu
WATEJA 76 wa DStv wamejinyakulia zawadi mbalimbali kutoka Multichoice
Tanzania katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Jishindie na DStv’ ambapo mteja wa
DStv anapata fursa ya kujishindia zawadi kwa kulipia king’amuzi chake kwa
angalau miezi miwili mfululizo.
Kati ya washindi hao 25 wamejipatia zawadi ya ving’amuzi vya
DStv Explora, ambavyo ni ving’amuzi vya kisasa kuliko vyote hapa nchini.
Washindi wawili wamejishindia Kifurushi cha Premium cha Tsh 169,000) cha mwezi,
wengine wawili Kifurushi cha Compact+ cha Tsh 109 000), huku washindi 10
wakishinda kifurushi cha Compact cha Tsh 69,000), 10 kifurushi cha Famili
(39,000) na wengine 25 Kifurushi cha Bomba cha Tsh 19,000.
Washindi wawili wa droo kubwa ambao ni Anicet Macheta wa Kagera
na Hassan Juma Hassan wa Dar es Salaam wamejishindia zawadi kubwa kabisa ambayo
ni safari ya kutalii visiwani Zanzibar wao pamoja na familia zao zisizozidi
watu waNne kila familia.
Akizungumza baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo katika ofisi
za Multichoiche Tanzania, Meneja wa Uhifadhi Wateja Hilda Nakajumo amebainisha
kuwa zaidi ya wateja 30,000 wameshiriki kwenye promosheni hiyo iliyoendelea kwa
miezi miwili.
Hilda amesema, wamefurahi kuona kuwa washindi takriban 200
waliopatikana wakati wote wa promosheni wametoka maeneo mbalimbali ya nchi
ikiwemo Arusha, Mwanza Dar es Salaam, Kagera, Iringa, Geita Kilimanjaro,
Kigoma, Mbeya, Morogoro, Ruvuma na mikoa mingine kote nchini.
“Wakati wote DStv tunahakikisha kuwa wateja wetu wanafurahia
huduma zetu kwani mbali na kwamba sisi ni vinara katika burudani na michezo,
pia tunakuwa na promosheni za mara kwa mara ambapo wateja wetu hupata zawadi
mbalimbali” alisema Hilda.
Amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa neema kwa wateja wa DStv
kwani mbali na kuongeza chaneli kwenye vifurushi hususani vile vya bei ya
chini, pia hivi majuzi DStv ilipunguza bei za vifurushi vyake vyote ili
kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata huduma hizo kwa unafuu mkubwa.
Kampuni ya Multichoice Tanzania inayoendesha biashara ya
vingamuzi vya DStv, ina umri wa miaka 20 sasa, ambapo ilianza shughuli zake
hapa nchini mwaka 1997.
No comments:
Post a Comment