|
Mhandisi Kerdick
Chawe (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (mwenye
ushungi) kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), wanaoshiriki kwenye maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika
kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.
|
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof.
Jumanne Maghembe leo Ijumaa atafungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini
kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim, yanayofanyika kwenye viwanja vya
Kichangani mkoani Iringa.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya Utalii
Endelevu ni Nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika taasisi za serikali,
mashirika ya umma na kimataifa zaidi ya 400, ambapo yatamalizika Oktoba 2,
2017, ambapo yanalengo la kuweka uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa utalii na
thamani thamani ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii kwa kuihamasisha jamii
kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wa Wizara mbalimbali zipo na
taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Idara ya
Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki, Chuo cha Taifa cha
Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa
Misitu Tanzania (TaFF).
|
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela
(kulia) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo
Kata ya Nduli, katika banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya
Kichangani mkoani Iringa. |
Taasisi nyingine ni Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania, (TFS) Taasisi ya
Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Wadau wa Sekta ya
Utalii kutoka mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu na mikoa inayoshiriki
ni pamoja na wenyeji Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe.
|
Ofisa Uhusiano wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Bahati Mollel akimkaribisha
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesera katika banda lao la maonesho ya
Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani
Iringa.
|
Fursa zilizopo nyanda za Juu Kusini ni
pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa,
Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya, Hifadhi za Mahale, Katavi,
Ruaha, Kitulo na Selous.
No comments:
Post a Comment