Saturday, 16 September 2017
Yanga yapambana na hali yake Songea
MABNGWA wa soka
Tanzania Bara Yanga jana walipambana na hali yao baada ya kutoka nyuma na
kulazimisha sare ya 1-1 na Majimaji katika mchezo uliofanyika mjini Songea.
Yanga
wamelalamikia Uwanja wa Majimaji kuwa ndio umesabaisha timu yao kutocheza
vizuri na kusababisha kuambulia sare hiyo katika mchezo huo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara.
Kocha msaidizi wa
Yanga, Shadrack Nsajigwa alilalamikia uwanja huo na kusema kuwa umechangia
kutopata ushindi, lakini aliipongeza Majimaji kwa sare hiyo.
Kocha wa Majimaji
Peter Mhina amewapongeza wachezaji wake na kusema kuwa walicheza vizuri huku
akisema bao la Yanga lilipatikana baada ya mabeki wake kufanya makosa ya
uzuiaji.
Mzimbabwe Donald
Ngoma ndiye aliyeiokoa Yanga isiondoke na kichapo baada ya kufunga bao la
kusawazisha katika katika dakika ya 79 kwa kichwa akimalizia krosi ya Mzambia,
Obrey Chirwa.
Majimaji ndio
ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Peter Mapunda katika dakika ya 54
akimalizia pasi ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete na kumfunga
kipa Mcameroon, Youthe Rostand.
Kipindi cha kwanza
wenyeji Maji Maji walitawala mchezo na kufika mara nyingi kwenye eneo la hatari
la Yanga, lakini hawakuweza kufunga.
Mchezo huo
ulisimama kwa muda katika dakika ya 39 baada ya Emmanuel Martin wa Yanga
kuzimia uwanjani baada ya kugongana na mchezaji wa Majimaji Mpoki Mwakinyuke.
Kwa sare hiyo
Yanga imefikisha jumla ya pointi tano baada ya kucheza mechi tatau, baada ya
kutoka sare mara mbili na kushinda mchezo mmoja huku Majimaji wakifikisha
pointi mbili baada ya kufungwa mechi moja na sare mbili.
Kikosi cha
Majimaji kilikuwa; Andrew Ntala, Juma Salamba, Mpoki Mwakinyuke, Kennedy
Kipepe, Tumba Sued, Hassan Hamisi, Suleiman Kassim , Yakubu Kibiga/Abdulhalim
Humud, Danny Mrwanda/Jerry Tegete, Marcel Kaheza na Peter Mapunda.
Yanga; Youthe
Rostand, Juma Abdul/Hassan Kessy, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kevin
Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Raphael Daudi, Donald Ngoma,
Ibrahim Hajib na Geoffrey Mwashiuya/Eammnuel Martin/Said Juma.
Katika mechi zingine jana; Mtibwa Sugar
iliifunga 2-1 Mbao FC huku Prisons ikitoka Suluhu dhidi ya Ndanda FC, Lipuli
nayo ikishindwa kutamba kwa Ruvu Shooting baada ya kulazimishwa sare ya bila
kufungana na Singida ilishinda 1-0 dhidi ya Stand United.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment