Monday, 25 September 2017
Mashabiki wa soka wafungwa maisha Misri
CAIRO, Misri
MAHAKAMA ya Misri
imewahukumu vifungo vya maisha watu wawili kutokana na vurugu zilizosababisha
vifo vya watu kibao kwenye Uwanja wa soka mjini hapa Februari 2015.
Angalau watu 19
walikufa uwanjani baada ya polisi kulipua gesi ya kutoa machozi kwa mashabiki
wakati wakijaribu kulazimisha kuingia kwenye Uwanja wa Jeshi la Anga.
Watuhumiwa wengine
12 walifungwa vifungo vya kati ya miaka miwili hadi 10 kwa kuhusu kwao katika
dhahama hiyo, ambapo wengine wawili waliachia huru.
Tukio hilo
lilitokea kabla ya mchezo kati ya Zamalek na
Enppi.
Mchezo huo ulikuwa
wa kwanza wa ligi kubwa nchini Misri kuruhusiwa mashabiki kuingia uwanjani
baada ya mashabiki kuzuiwa kushuhudia mechi kutokana na watu zaidi ya 70 kufa
uwanjani huko Port Said mwaka 2012.
Watuhumiwa hao
walikuwa wakikabiliwa na makosa ya mauaji, kuleta vurugu, na walikuwa
wakishtakiwa kukombana na polisi, na kusababisha vurugu.
Pamoja na wawili
kufungwa maisha, watatu walifungwa miaka 10, watano wamefungwa miaka saba,
watatu walifugwa jela miaka mitatu kila mmoja na mmoja alifungwa miaka miwili.
Washtakiwa wote
walikuwpo mahakamani wakati wa hukumu hiyo na ruksa kukata rufaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment