LONDON, England
KIUNGO Philippe Coutinho (pichani) ameachwa nje ya kikosi cha Liverpool
ambacho kesho kitakwaana na Manchester City katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya
England.
Mchezo huo utapigwa mapema kuanzia saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kwenye
dimba la Etihad.
Coutinho, 25, amerejea klabuni baada ya mara mbili akitokea
benchi alipoichezea Brazil katika mechi za kufuzu kwa Kombela Dunia 2018.
Mchezaji huyo alikosa mechi za Liverpool za mwanzo wa msimu
kutokana na maumivu ya mgongo pamoja na kutaka kuhamia Barcelona.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema: "Nimeamua
kutomjumuisha katika kikosi changu kitakachocheza na Man City ili aweze kutumia
muda kwa ajili ya mazoezi zaidi. Alikubali.”
Klabu hiyo ilitupilia mbali ofa tatu kutoka kwa vigogo vya
soka vya Hispania, Barcelona ambao walikuwa wanataka kumsajili Coutinho –
aliyeomba uhamisho, ambapo klabu hiyo ilisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi.
Alifunga katika ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kufuzu
kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador Ijumaa ya wiki iliyopita, na pia aliingia
kitokea benchi katika mchezo wa Jumanne walipotoka sare ya 1-1 na Colombia.
Mechi zingine leo zitakuwa kati ya Southampton itakayoikaribisha
Watford kwenye Uwanja wa St.
Mary's kuanzia saa 11:00 jioni, huku Brighton & Hove Albion ikicheza dhidi
ya West Bromwich Albion.
Everton wenyewe
watakuwa wageni wa Tottenham Hotspur katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa
Goodison Park huku Arsenal itakuwa na
kibarua dhidi ya AFC Bournemouth kwenye Uwanja wa Emirates.
Mabingwa wazamani Leicester City watawakaribisha mabingwa
watetezi, Chelsea kwenye Uwanja wa
King Power, huku Stoke City watakuwa wenyeji wa Manchester United.
No comments:
Post a Comment