Na Mwandishi Wetu
TIMU ya netiboli ya Uhamiaji imeanza vizuri
kampeni zake ya kutetea taji la Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya
kuifunga Polisi Morogoro 37-34 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo
cha Ushirika mjini Moshi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha
Netiboli Tanzania (Chaneta) Annie Kibira, Polisi Morogoro ilikuwa mbele kwa
mabao 21-17 na kuonekana kama ingeibuka na ushindi katika mchezo huo kabla ya
mambo kuwageukia kipindi cha pili.
Naye kocha wa Uhamiaji, Winnie Emmanuel
alisema kuwa mashindano ni magumu lakini wamejiandaa kuhakikisha wanatetea taji
lao vizuri.
Emmanuel aliwataka wapenzi wa michezo wafike
kwa wingi kushuhudia uhondo kutoka kwa Uhamiaji ambayo imejiandaa vizuri
kulitetea taji lao walilolitwaa mwaka jana.
Hatahivyo, alisema kuwa kuna sababu kadhaa
zilizoifanya timu yake kushindwa kuibuka na ushindi mnono, ikiwemo hali ya
hewa, kubaki nyuma kwa baadhi ya wachezaji wao kwa sababu ya majukumu ya
kikazi.
Annie Kibira. |
Alisema kuwa wachezaji hao wanatarajia
kuwasili kesho mjini Moshi, ambapo anatarajia watakiongezea nguu kikosi chao
katika mashindano hayo.
Uhamiaji kesho itacheza dhidi ya Madini ya
Arusha huku ndugu wawili, Polisi Moro watashuka dimbani kucheza dhidi ya Polisi
Arusha.
Mechi zingine za kesho ni pamoja na Polisi
Arusha itakayopepetana na Jeshi Stars wakati Arusha Queens itacheza dhidi ya
dada zao wa Madini, JKT Mbweni watacheza na Tanga Jiji.
Polisi Morogoro itacheza na Madini katika
moja ya mechi za jioni zitakazofanyika wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment