TIMU ya soka ya Mawenzi Market ya Manispaa ya
Morogoro inayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara imeshindwa
kutamba katika uwanja wake wa nyumbani baaada ya kufungwa na KMC ya Kindondoni,
Jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-1.
Licha ya
kipindi cha pili Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini, Abdulaziz Abood
kuwaahidi wachezaji donge nono la Sh 800,000 endapo wangeshinda mchezo huo huku
ikiwa nyuma kwa bao 1-0 hadi mapumziko
ilishindwa kunyakua kitita hicho kwa
kupoteza mchezo huo kwenye uwanja wa nyumbani wa Jamhuri wa mjini Morogoro.
Bao la kwanza la Kinondoni ilipachikwa dakika ya nne
na mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga
Stephen Mwasika na lilidumu hadi
mapumziko, ambbapo kipindi cha pili
dakika ya 51 vijana wa Mawenzi Market walisawazisha bao hilo kupitia mchezaji
Maulid Iddi kwa shuti hafifu baada ya mpira wa adhabu uliookolewa na beki wa
Kinondoni kumkuta mfungaji.
Timu ya Kinondoni ambayo ilikuwa na baadhi ya
wachezaji wenye uzoefu wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza ikiwa na Kocha Mkuu , Fred Felix Minziro ‘ Majeshi’ ilibadili mfumo wa uchezaji wa pasi fupi na
kutumia pasi ndefu uliowezesha kupata
bao la pili na la ushindi katika dakika ya 86 kupitia Cliff Athony baada ya
mpira uliopingwa na Mwasika kugonga mwamba na kumkuta mfungaji huyo.
Hadi dakika 90 za mchezo huo vijana wa KMC kutoka Kinondoni Jijini Dar es Salaam waliibuka kidedea kwa
ushindi wa mabao 2 -1 dhidi ya Mawenzi Market.
No comments:
Post a Comment