Wachezaji, viongozi na waamuzi wakicheza kwaito baada ya kumalizika kwa mashindano ya riadha ya Kanda ya Tano ya Afrika yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
|
Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imeshika nafasi ya kwanza katika mashindano
ya riadha ya Kanda ya Tano ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18
kwa upande wa wanawake huku ikishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla katika
mashindano hayo yaliyomalifika jana kenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Michezo nchini, Yusuph Singo akimvisha medali mmoja wa wanariadha wa Zanzibar walioshiriki mbio za kuokeana vijiti na kutwaa nafasi ya tatu.
|
Pia wanariadha 13 wa Tanzania ia wamefuzu kushiriki
mashindano ya dunia ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 yatakayofanyika
Kenya Julai mwaka huu baada ya kukimbia muda mzuri katika mbio zao.
MATOKEO YA WASICHANA, WAVULANA NA WASHINDI WA JUMLA
Kwa upande wa wanawake, Tanzania ilitwaa medali tano
za dhahabu, nne za fedha na tatu za shaba, ikifuatiwa na Kenya akati Sudan
ilimaliza ya tatu, Zanzibar ya nne, Eritrea ya tano, Sudan Kusini na Somalia zilifungana
katika nafasi ya sita kwa upande huo wa wanawake.
Magwiji wa riadha nchini, Filbert Bayi (kulia) na Juma Ikangaa wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya riadha ya Kanda ya Tano ya Afrika kwenye Uwanja wa Taifa. |
Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijafanya vizuri
katika mashindano ya riadha kama timu, jana katika mashindano hayo ya vijana kwa
ushindi wa jumla, ilijukusanyia medali saba za dhahabu na fedha saba, huku tatu
zikiwa za shaba.
Timu ya Tanzania ya mchezo wa mbio za kupokezana
vijiti kwa wavulana ndio ilimalizia medali za dhahabu baada ya kushika nafasi
ya kwanza huku wasichana wao wakimaliza a pili nyuma ya Wakenya na kupata
medali ya fedha.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja akimvisha medali mwanariadha wa Tanzania.
|
Kama timu ya kupokezana vijiti ya wasichana ya mchezo
wa meta 400 x 4 ingepata medali ya dhahabu, basi Tanzania ingekuwa mshindi wa
kwanza wa jumla, lakini sasa Kenya ndio ilitwaa ushindi wa jumla wa mashindano
ya mwaka huu.
Kenya imeshika nafasi ya kwanza baada ya kutwaa
medali nane za dhahabu, nne za fedha ba tatu za shaba wakati Zanzibar ilimaliza
ya tatu baada ya kutwaa medali nne za dhahabu, fedha tano na shaba nne.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Sudan ilimaliza ya nne
kwa kutwaa medali mbili za dhahabu, tatu za fedha na mbili za shaba, wakati
Eritrea ilishika nafasi ya tano kwa kuwa na medali tatu za fedha na sita za
shaba huku ikiwa haina medali hata moja ya dhahabu.
Sudan Kusini ilimaliza ya sita baada ya kuambulia
medali moja tu ya shaba wakati Somalia ilishika mkia baada ya kushindwa
kuambulia medali yoyote ile.
Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya nchi saba,
ambazo ni wenyeji Tanzania, Zanzibar, Kenya, Eritrea, Sudan, Sudan Kusini na
Somalia wakati nchi ambazo hazikufika ni pamoja na Rwanda, Uganda, Ethiopia na
Djibout.
Mashindano hayo ambayo yalifunguliwa juzi na Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, yalifungwa jana na
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Mohamed Kiganja.
No comments:
Post a Comment