Na Mwandishi Wetu
Siku chache baada ya DStv kutangaza
kuwa itarusha moja kwa moja (Mubashara) Michuano ya vijana ya AFCON itakayoanza
kesho huko Gabon, habari mpya na njema zinasema sasa DStv itarusha mechi zote
za Serengeti boys katika michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice
Tanzania Maharage Chande, amesema baada ya kampuni yake kuhakikisha kuwa
michuano hiyo inashuhudiwa mubashara kupitia DStv, sasa wanataka watanzania
wengi zaidi waweze kuifuatilia kwa karibu hususan mechi za timu yetu ya
Serengeti Boys, hivyo mechi zote za Serengeti boys zitarushwa mubashara kwa
lugha ya Kiswahili.
Amesema watangazaji na wachambuzi
mahiri wa mpira wakiwemo Abuubakar Lyongo, Maulid Kitenge, Ephraem Kibonde, Edo
Kumwembe na Maestor watashiriki katika zoezi hilo la kuwaletea watanzania
burudani hiyo kupitia DStv.
“DStv tunatoa huduma wanayotaka wateja
wetu, tunawasikiliza wateja wetu, na kila inapowezekana tunatekeleza matakwa
yao” alisema Maharage na kuongeza kuwa baada ya watu kufahamu kuwa DStv
itarusha michuano hiyo mubashara, kumekuwa na maombi mengi ya kuangalia
uwezekano wa kutangaza michuano hiyo hususan mechi za Serengeti boys kwa
Kiswahili.
“Tunaamini kuwa kwa kurusha matangazo
hayo kwa Kiswahili, watanzania wa kila kada wataweza kuifuatilia michuano hiyo
kwa ukaribu zaidi na hivyo kuongeza burudani ya aina yake katika michuano hiyo”
alisema Maharage na kuongeza kuwa pamoja na kutangaza kwa Kiswahili, pia wamehakikisha
michuano hiyo inaonekana katika vifurushi vyote kikiwemo cha Bomba cha Sh.
19,975tu ambacho ni miongoni mwa vifurushi nafuu kabisa hapa nchini.
Amewataka watanzania wote kuendelea
kuiunga mkono timu yetu kwa kila hali kwani ni muwakilishi wa taifa letu katika
michuano hiyo muhimu. “Sisi DStv ni wazalendo wa kweli, ndiyo sababu hatusiti
kuunga mkono timu zetu wakati huohuo tukiwahakikishia watanzania fursa ya
kushuhudia mashindano mbalimbali mubashara. Enzi za kuangalia micezo
iliyonakiliwa imepita, na sisi watanzania tunaenda sambamba na ulimwengu wa
kisasa. Kupitia DStv, tunaona vitu mubashara” alisema Maharage.
Serengeti Boys watacheza mechi yao ya
kwanza siku ya Jumatatu 15 Mei kabla ya kukabiliana na Angola siku ya Alhamisi
18 Mei na hatimaye Niger siku ya Jumapili 21 Mei.
Kwa mujibu wa majadiliano mbalimbali
kwenye mitandao ya kijamii, watanzania wengi wanasubiri kwa shauku michuano
hiyo huku ikionekana wazi kuwa wanaimani na Serengeti boys.
Michuano ya AFCON kwa wachezaji wenye
umri wa miaka chini ya 17 ya mwaka huu ni ya 12 kwa kuzingatia michuano
inayohusisha nchi waandaaji, inayoandaliwa na shirikisho la soka barani Afrika
(CAF) kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17. Washindi wane watapata tiketi ya kushiriki
michuano ya Kombe la Dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 17
litakalofanyika ncini India mwishoni mwa mwaka huu.
Michuano ya mwaka huu awali ilipaswa ifanyike
nchini Madagascar tarehe Aprili 2–16, lakini Shiirikisho la Soka la Afrika, CAF, l ikaamua kuihamishia Gabon
kwa sababu Madagascar haikukidhi vigezo.
Mataifa yaliyofuzu kushiriki michuano hii mwaka huu ni wenyeji Gabon, Tanzania, Mali, Angola, Cameroon,
Ghana, Guinea, na Niger.
Wasalaam,
Shumbana James
No comments:
Post a Comment