LONDON, England
PAMOJA na kushinda mabao 3-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa mwisho wa
Ligi Kuu ya England, Arsenal imeshindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya
tano.
Timu hiyo ambayo ilianza siku ikiwa pointi moja nyuma ya Liverpool
iliyokuwa katika nafasi ya nne, ilionekana kama ingeweza kumaliza ya nne baada
ya kupata bao la kuongoza katika dakika ya nane.
Lakini Liverpool, ilihitaji ushindi tu wa aina yoyote ili imalize katika
nafasi ya nne, ambapo ilianza kuifunga Middlesbrough kabla ya mapumziko na
kuibuka na ushndi wa mabao 3-0.
Manchester City yenyewe ilimaliza ya tatu baada ya kupata ushindi rahisi
wa mabao 5-0 dhidi ya Watford.
Ligi ya Ulaya kwa Arsenal
Hatua ya Arsenal kufuzu kucheza Ligi ya Ulaya kwa mara ya 19 mfululizo
ilifikia tamati jana baada ya kumaliza katika nafasi ya tano.
Imani ilikuwepo kwa mashabiki wa nyumbani wakati Hector Bellerin
alipoifungia the Gunners bao la mapema huku taarifa zikizagaa kuwa, Liverpool
ilikuwa katika wakati mgumu dhidi ya wapinzani wao Hull City ambao tayari
walishashuka daraja.
Liverpool sasa itacheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza
tangu ilipofanya hivyo kwa mara ya mwisho msimu wa mwaka 2014-15.
Manchester City ilitwaa nafasi ya tatu na kufuzu moja kwa moja kucheza hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kushinda 5-0 dhidi ya Watford.
Mabingwa Chelsea imekuwa timu ya kwanza ya Uingereza kushinda mara 30
katika ligi kubwa katika mechi 38 za msimu mmoja wakati timu hiyo ikimuaga
nahodha wao wa muda mrefu, John Terry huku ikipata ushindi mnono wa 5-1 dhidi
ya Sunderland.
The Blues, ambayo imetwaa ushindi wake wa sita wa Ligi Kuu siku tisa
zilizopita, ilijikuta nyuma baada ya bao la mapema la Javier Manquillo lakini
ilijibu mapema kupitia Willian.
Eden Hazard alifunga bao lake la 17 la msimu na kuifanya timu yake
kuongoza kabla nafasi yake haijachukuliwa na Pedro.
Katika mechi zingine za ligi hiyo, Burnley ilifungwa na West Ham mabao
2-1 huku Hull City ikipokea kichapo cha mabao 7-1 kutoka kwa washindi wa pili
wa ligi hiyo, Tottenham.
No comments:
Post a Comment