Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya Eritrea imesema kuwa itafanya vizuri katika mashindano
ya riadha ya Kanda ya Tano ya Afrika yatakayoanza Jumamosi kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa msafara wa timu hiyo, ambaye pia ndiye rais wa Shirikisho la
Riadha la Eritrea, Bereket Mesfun alisema jana jijini kuwa, timu yao imejiandaa
vizuri na imekuja kushinda.
Alisema hali ya hewa ya sasa ya Dar es Salaam wameifurahia sana na
inafana na ile ya kwano, hivyo itawasidia kufanya vizuri pia.
Naye Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Wilhelm Gidabuday alisema kuwa
jumla ya nchi saba zitashiriki katika mashindano hayo badala ya 11 za awali.
Gidabuday alizitaja nchi zilizothibitisha kuwa ni pamoja na Eritrea,
ambayo tayari imetua nchini na Sudan Kusini ilitarajia kuwasili jana kwa njia
ya barabara.
Nyingine ni Kenya, Sudan, Zanzibar, Somalia pamoja na wenyeji Tanzania
Bara, ambayo timu yao leo itahamishia kambi jijini Dar es Salaam kutoka Kibaha
tayari kwa mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment